Unapata shida? Wasiliana nasi kwa +255 762 204 166

Ingia

Karibu Tena, Rafiki. Ingia kuanza kusoma vitabu

JISAJILI

Ukimaliza kujisajili hapa, lipia riwaya kwa M-pesa!

Kurudisha Neno la siri

Forget your password? Don't worry we can deal with it

UTANGULIZI - SAA 72S A A 7 2
Februari 25, 2003

Bogoro – Buni, DRC

Msichana wa miaka 15 hivi, akiwa na majeraha mazito mwilini alizidi kujilazimisha kupiga hatua kwenye mtaa uliojaa maiti. Majeraha yake yaliyokuwa bado mapya yalifanya ausikie mwili wake kuwa kama ganda la kidonda kilichooza ambacho kilikuwa kikingoja mkasi kutumbuliwa ili kirushe usaha mzito. Kwa hali ilivyokuwa hakuwa na wakati wala namna ya kuyapooza majeraha yake hayo.
Kila kitu kilikuwa kimeharibika, nafsi yake ilikuwa imechafuka, akili yake ilikuwa imevurugwa vibaya, uwezo wake wa kufanya maamuzi ulishakufa ganzi.
Hali yake ya utu ilikuwa imeng’olewa kwa vile alivyokuwa amelazimika kuua bila kujali ili kupigania maisha yake, maana maisha huwa na thamani kubwa sana mtu anapokuwa kwenye mdomo wa mauti, ndio maana hata mgonjwa aliyedhoofu sana utashangaa anapata wapi nguvu anazotumia kupigania pumzi ya mwisho. Ni wakati mtu anapotakiwa kutoa pumzi ya mwisho ndipo huwa tayari kufanya chochote ili pumzi hiyo isimtoke!
Hakuwa akijali kitu sasa, bunduki aina ya SMG ikiwa inaning’inia begani kwake alishitushwa na mlio mkali wa ndege aina ya Tai aliyekuwa akiruka kwenye anga la eneo alilokuwepo.

Ndege huyu aina ya Tai alikuwa amefungua mabawa yake na kuyaachia yamiliki anga lililo juu ya kijiji kidogo kilichoko kwenye vilima vya Ituri, kijiji hicho kinaitwa Bogoro. Kiko kilomita kama 25 hivi toka mji wa Buni, Congo DRC. Tokea angani, macho yake makali yalikuwa yakiangalia juu ya barabara za mitaa ya mji huo, maiti kadhaa zilionekana zikiwa zimetapakaa mitaani. Ndege huyo fundi na mbabe wa anga, alitikisa mkia wake kwa furaha huku akitoa ukelele wa kusheherekea hali aliyoiona mitaani. Maiti zilizotapakaa, hali ya baridi na unyevunyevu kufuatia mvua iliyokuwa imekatika punde, ilileta upweke kwenye mitaa hiyo ya Bogoro.

Kwa kawaida mji wa Ituri hufunikwa na mvua kubwa tangu mwezi wa pili hadi mwezi Juni. Mji huu ambao una lile pori kubwa na maarufu lenye mvua nyingi sana lijulikanalo kama msitu wa Ituri huwa wa kijani kibichi muda wote wa mwaka. Ndege walikuwa wenye furaha, mijibwa ya mitaani ilikuwa imetulizana huku ikiwa imeshiba. Mlio wa maji yaliyokuwa yakitiririka baada ya mvua kubwa ulisikika. Hali ilikuwa kimya kabisa huku magari kadhaa-machache sana ya jeshi yalionekana kuzunguka kila baada ya dakika kadhaa. Magari hayo yalikuwa yameandikwa FRPI kifupi cha Patriotic Resistance Force in Ituri. Kwa ujumla hali ilikuwa ukiwa sana. Katikati ya hali hiyo Tai huyo aligeuza kichwa chake kumtazama binti mdogo aliyekuwa akikatiza kwenye mitaa pweke ya eneo hilo. Mitaa iliyokuwa imejaa maiti nyingi, zilizokuwa ama na majeraha mabaya ya risasi au visu. Hii ilikuwa ni masaa machache tangu yalipohitimishwa yale mauaji ya kikabila ya Bogoro ambayo wenzetu waliyabatiza jina ‘Bogoro massacre’. Msichana huyu, alitembea taratibu huku akitetemeka kutokana na jinsi hali ilivyokuwa. Alitembea hivyo huku akijificha ficha. Tai yule alijikuta akimshangaa binti huyo, hivyo akawa akiruka anga hilo na kutoa milio ya kipekee huku macho yake makali yakimdhihaki.
Binti mwenyewe alimuangalia yule Tai kwa jicho baya, alitamani angekuwa na uwezo wa kumnyamazisha lakini alijua hilo lilikuwa nje ya uwezo wake, alizidi kwenda kwa kujificha ficha huku akijitahidi kujificha kwenye macho ya yule Tai, kutokana na uzoefu wake binti huyo, Tai huyo alikuwa wa hatari kama ambavyo magari ya wanajeshi yaliyokuwa yakipita yalivyokuwa ya hatari. Akiwa na umri wa miaka 15, tayari alikuwa amefunzwa vema kama mwanajeshi kamili, alikuwa na uwezo huo japo hakuwa na muonekano huo, akiwa anatokea kwenye kabila la Lendu, kabila ambalo hujishughulisha na kilimo kwenye eneo hilo la Ituri, kufunzwa vita ilikuwa sehemu ya lazima kwenye jamii, hii iliwawezesha kuwa tayari kwa vita ya kikabila kati ya kabila lake yaani Lendu na ile ya Hema. Makabila yote haya mawili yalikuwa yakipatikana kwenye jimbo hilo la Ituri, huku Lendu wakijihusisha zaidi na kilimo na kabila la Hema wao wakifanya zaidi ufugaji. Ufugaji na ukulima ndio ilikuwa chanzo kikubwa cha kupigana kwao, hawa wakitaka sehemu za malisho na hawa wakitaka sehemu za kulima.
Yeye akiwa kati ya watoto waliokuwa wamekamatwa kwa nguvu na kufundishwa mapigano na kundi la kijeshi la FRPI lililokuwa likiongozwa na Joseph Katanga. Ilikuwa dhahiri kichwani mwake kuwa mlio wa yule Tai, ungetuma ujumbe tosha kwa mwanajeshi yeyote kuwa eneo lile kulikuwa na mtu aliyeonekana wa ajabu ajabu, ndio maana hakupenda kuona yule Tai akiendelea kuzunguka eneo lile na kutoa aina ya mlio aliokuwa akitoa. Baridi kali, ubichi-ubichi, maiti za watu, upweke, majeraha aliyokuwa nayo na njaa vilifanya aonekane kiumbe wa ajabu katikati ya uwanja wa mauti.
Huku akiwa anachechemea, mara hii akaingiza mkono wake tena kuelekea sehemu za siri. Alipoutoa bado aliweza kuona damu mbichi kabisa ikiwepo, alisimama, akavua chupi aliyokuwa amevaa, aliiangalia ile chupi jinsi ilivyokuwa imechanwa kwa fujo na mtu aliyekuwa katika zoezi la kumbaka. Hapo machozi yakaanza kumtoka kwa mara nyingine tena, aliitupa chini ile chupi na kuendelea kutembea taratibu huku akichechemea kufuatia majeraha mwilini, baridi lakini pia kitendo cha kubakwa na mtu aliyekuwa amemuamini sana. Joseph Katanga. Hakutegemea kuwa siku mmoja kiongozi wao wa kundi la kijeshi, mtu aliyekuwa akihubiri kuwa alikuwa anapigania na kutafuta haki ya kabila la Lendu na jamii ya wakulima kwa ujumla angembaka kinyama namna ile. Khajat, huku silaha yake aina ya SMG ikiwa begani, silaha ambayo ilionekana kumzidi umri, alikuwa akikatisha upande mmoja wa barabara kwenda mwingine wakati aliposikia muungurumo wa gari ukija. Wakati huo huo yule Tai alizidi kupiga kelele, alikimbia na kwenda kujibanza nyuma ya kibanda fulani cha mbao. Ni wakati akiwa na hakika kuwa amejificha vema ndipo aliposikia sauti upande mwingine ikisema ‘Khajat, not safe, run this way! (Khajat, siyo salama, kimbilia huku!). Ilikuwa ni sauti ya mtu aliyemjua, lakini haikuwa sauti ya mtu aliyetegemea kukutana naye. Aliangalia kule ilikotokea ile sauti, akamuona mtu aliyemuita, alimuangalia jinsi alivyokuwa taabani, akajikuta anashawishika kwenda kumsaidia, wakati anakwenda akasahau kuwa alikuwa amesikia mlio wa gari hapo kabla, kutokana na ukaribu wa yule mtu aliyemuita na jinsi alivyokuwa amejeruhiwa akakimbia tena kuvuka barabara. Wakati huo huo akasikia mvumo wa gari ukiwa jirani kabisa na alipokuwa, lakini kabla gari ile haijamfikia, ulitokea mlipuko mkubwa toka kwenye kile kibanda alichokuwa amejibanza. Mlipuko uliomrusha hewani, akiwa hewani, msichana yule alitoa ukelele mkubwa wa hofu na maumivu “Jooooaaan!!”

“Noooo, Khajat!!” Huyu aliyejulikana kama Joan alipiga kelele baada ya kuona Khajat ametua chini kama mzigo baada ya kuwa amerushwa juu. Wakati anataka kukimbilia pale alipokuwa ameangukia Khajat, Joan alishikwa na mshangao alipomuona mzee mmoja wa makamu akienda pale alipoangukia Khajat na kumchukua. Ilikuwa ni kitendo cha kasi na wepesi sana. Ilikuwa kama vile Mwewe amchukuavyo kifaranga. Yule mzee alitowekea kwenye majengo yaliyokuwa jirani. Kuona hivyo Joan akakimbilia sehemu ambayo mzee yule alikuwa ameingia na Khajat. Vilikuwa ni vitendo vya haraka, hivyo wakati Joan naye akiwa anapotelea kwenye lile jengo ndipo gari la jeshi la FRPI lilipopiga breki kwa fujo eneo hilo. Wanajeshi kadhaa walishuka na kuanza kukimbilia alipokuwa ameelekea Joan.
“Shiiiiiiii!” Yule mzee alisema mara baada ya Joan kutokezea kwenye chumba ambacho alikuwa amemlaza Khajat na kuanza kumpa huduma ya kwanza.
“Mzee Kasheba!” Joan alisema.
“Kaa hapo Joan, huyu anahitaji huduma ya haraka kama kweli tunataka aendelee kuishi!” Alisema mzee Kasheba.
“Wako wanakuja huko nje!” Joan alisema. Punde kidogo wakasikia mlango wa jengo hilo ukigongwa kwa nguvu.
“Oooooh shiiit!” Mzee Kasheba alisema kwa mshituko.

* * *

“Wote wako hapa isipokuwa watu wawili tu ndio wanakosekana!” Alisema askari huyu mwenye cheo cha juu jeshini huku jicho lake moja la kushoto likiwa na bandeji nyeupe iliyochafuka damu.
“Umeshajua ni nani wanaokosekana? unajua inatakiwa tukamilishe kazi hii ndani ya masaa machache yajayo!!” Alisema Joseph Katanga, ambaye alikuwa amechafuka sana, mavazi yake ya kijeshi yakiwa na matone na michirizi mingi ya damu.
“Kwa orodha iliyokuwa imetolewa mwezi wa nne siku chache kabla operesheni hii haijaanza wanaokosekana hapa ni Khajat na Joan!” Alisema huyu mwanajeshi mwenye jicho lenye bandeji.
“Watafutwe, hii ni sumu ambayo hapo baadaye itatuathiri, halafu nataka kujua kwa nini wao hawakuwa na watu wa kuwachukua wakati mambo yalipoanza?” Alisema Joseph Katanga. Wakati wakiongea hayo mara akaingia mtu mwingine aliyekuwa amevaa kiraia, wote wakampigia saluti. Hakujisumbua kuitikia saluti zao, alikuwa jamaa mrefu, mzungu, mwenye kipara kinachong’aa, aliwaangalia kwa muda bila kusema neno, halafu akatoa tabasamu la dhihaka. Hapo meno yake yaliyoungua na jino moja la dhahabu pembeni vilionekana.
“Nasikia kuna wasichana wawili wamekosekana, jitahidi watafutwe haraka, nataka hili jambo limalizike ndani ya muda mfupi ujao ili tumiliki mambo kama tulivyopanga” Alisema huyo mtu mwenye meno machafu kwa ghadhabu.
“Tayari tumeshawaombea hifadhi Tanzania, hivyo tunangoja hao wawili wapatikane ili malengo yetu yatimie, nawapa masaa kumi na mbili muwe mmekamilisha” Alisema huyo mzungu aliyejulikana kwa jina la KK na kutoka nje ya chumba kile huku nyuma akiwaacha Joseph Katanga na askari mwingine.
“Tumeua zaidi ya watu 200 usiku wa kuamkia leo, hebu hivi vitoto visituharibie kazi, huyo Joan ni mjukuu wa mzee Kasheba. Hebu nenda kaangalie, kama wako kwake muue yeye halafu walete, sitojali ukweli kuwa ni rafiki yangu lakini kama hafuati nisemacho sheria hufuata mkondo wake. Fanya haraka nataka kufunga kazi hii haraka iwezekanvyo, halafu nianze kuangalia kwenye TV jinsi suala hili litakavyoongelewa!” Katanga alisema huku macho yake yakionekana kuwa machovu na mekundu, hii ni kutokana na kazi aliyokuwa ameifanya usiku kucha. Kazi ya kuongoza jeshi la FRPI kuwaua watu wote wa jamii ya Hema na kuhakikisha hakuna mfugaji anabaki eneo hilo. Lilikuwa ni zoezi kubwa na gumu, waliua kadiri walivyoweza na kwa namna yoyote ile.
Yule askari alipiga saluti na kuondoka na vijana wengine kumi, walielekea nyumbani kwa Mzee Kasheba kuona kama wanaweza kuwapata Joan na Khajat.

Goma, DRC – 2017

Alhamisi, Saa 4:30 usiku

NDEGE maalum iliyokuwa imebeba makomandoo watano, ilikuwa ikipita juu ya anga la Goma - Congo DRC, anga lililokuwa limefunikwa na mawingu mazito, meusi ambayo mara kwa mara yalikuwa yakimulikwa na mwanga wa radi. Ndege hiyo ilikuwa na jumla ya abiria sita pamoja na rubani, japo ilikuwa na uwezo wa kubeba abiria kumi na mmoja. Makomandoo wote walikuwa na vifaa vyao tayari kwa kuruka toka kwenye ndege hiyo hadi kwenye kambi maalum ya jeshi la serikali ambayo ilikuwa eneo hilo la Kivu Kaskazini.
Ilipofika eneo fulani, ndege hiyo maalum ilitoa mlio maalum, hivyo makomandoo wote wakajua walikuwa wamefika sehemu waliyotakiwa kudondoshwa, kila mtu akaanza kuweka sawa begi lake wakati ndege hiyo ilipokaribia sehemu ambayo makomandoo hao wangedondoshwa kwa miavuli.
“Haya makamanda tuko eneo husika. Nitahesabu hadi tano, kisha nitafyatua mlango nanyi mtaruka, mlango utakuwa wazi kwa sekunde thelathini halafu nitaufunga. Kila la kheri makamanda!” Kapteni Ambrose ambaye ndiye alikuwa rubani wa ndege hiyo alisema kwa sauti ya juu.
Makomandoo walikuwa kimya kila mmoja akiwa tayari kwa tukio.
“Moja…mbiliii…tatuuu…nnneeee… Tano twendeeee!”
Mlango ulifyatuka makomandoo wakajiachia hewani.
Ilitokea kama ghafla tu neno “shiiiiiit!” likasikika.
“Nini tena?” Kapteni Ambrose alihoji kwa hamaki baada ya kusikia komandoo mmoja akisema shiiiit!
“Limechanika, anyway ngoja niende, see you Captain!” alisema komandoo huyo aliyekuwa amesema shiit hapo awali, baada ya kubaini kuwa parachuti lake lilikuwa limechanika sehemu ya katikati.
“High risk (ni hatari sana), ngoja kidogo!” Kapteni Ambrose alipiga kelele kumzuia yule komandoo asiruke, lakini alikuwa ameshachelewa, yule komandoo alikuwa ameshajiachia angani!

* * *Alhamisi, Saa 5:15 usiku

Komandoo wa kwanza alitua kwa kukimbia kwenye shamba kubwa la kahawa, zao ambalo ni maarufu eneo hilo. Dakika tano baadaye makomandoo wote isipokuwa mmoja tu walikuwa wameshafika sehemu waliyokuwa wakitarajiwa kutua. Hapo walipokelewa na wanajeshi watatu wenye vyeo vya juu wa jeshi. Makomandoo waliopokelewa ni Twaha Mchopa, Musa Buti, Mark Muga na Emily Otieno.
“Poleni kwa safari!” alisema afisa mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Meja Jean Francis Kabananga.
“Asante. Ila tuna wasiwasi na mwenzetu sijui amepatwa na madhila gani!”
“Nilitaka kuuliza, maana tuliambiwa mko watano!?” Meja Kabananga alisema
“Tulimsikia akilalamika akiwa angani, nadhani alipata changamoto ndogo, ila yeye ni muhitimu bila shaka atafika tu,..” Luteni Musa Buti, mmoja wa wale makomandoo alisema. Yeye ndiye kiongozi wa wenzie kwenye misheni hii.
“Kwani hapatikani kwenye mawasiliano?” Meja Kabananga alihoji wakati wakielekea kwenye magari matatu ya kijeshi yaliyokuwa yamepaki eneo hilo.
“Dakika tatu baada ya kutua tulikuwa na mawasiliano naye, akatuambia kwa sababu ya kuharibika parachuti lake amedondokea mbali na sehemu iliyokusudiwa, na kama unavyoona hali hii ya upepo mkali na mvua hizi bila shaka unaweza kuelewa mtu akikutwa na ajali ya kuharibikiwa parachuti angani!” alisema Luteni Musa Buti.
“Okay, maadam ana ramani tutamngoja hapo kambini, ni kilomita kumi toka hapa, twendeni maana mnasubiriwa kwa hamu kubwa sana na mkuu!” Meja Kabananga alisema kwa Kiswahili chake cha Kikongo. Mvua nzito ilikuwa bado ikiendelea kunyesha, milio ya bunduki na risasi vilisikika kwa mbali, kitu kilichowaambia wale makomandoo kuwa walikuwa wameingia kwenye uwanja wa vita.
“Nasikia milio ya mashine huko!” Mchoppa alisema
“Nakwambia hapa limeshakuwa swala la kawaida wakati wote ni wakati wa mapambano, hali iliyofanya raia na askari wazoee tu sasa!” Alisema afisa mmoja wa jeshi. Ardhi ilikuwa imelowa chepechepe.


Alhamisi, Saa 5:15 usiku.

Kilomita nane toka mahali ambapo Meja Kabananga alikuwa anawapokea wale makomandoo, huyu naye alikuwa amepokelewa kwa namna yake. Baada tu ya kutua chini, Komandoo Pablo Mahene alishtukia anamulikwa na mwanga mkali sana usoni. Wakati bado anahangaika namna ya kujitoa kwenye parachuti alishtukia anachomwa na kitu kama sindano shingoni. Fahamu zikamtoka.
“Ndio mkuu, kama tulivyotarajia, aliangukia eneo lilelile,” alisema jamaa mmoja mrefu sana, mweusi sana, mwenye jicho moja bovu, wakati huu walikuwa kwenye gari moja la jeshi lililokuwa likiendeshwa kwa kasi sana kama wako kwenye barabara ya lami.
“Vema, kazi nzuri! Sasa watajua kuwa Jose Katanga karudi, watafidia muda wote ambao nilikuwa nje ya uwanja!” Ulisema upande mwingine kwenye redio ile ya mawasiliano.
“Haya ndio mambo tulikuwa tunayakosa bosi, huu msisimko umerejea tena!” Alisema yule jamaa mrefu, mweusi, mwenye jicho bovu.
“Mwiteni mzee Kasheba amuhoji huyo jamaa!” Joseph Katanga alisema.

1


“T u n a S a a 72 T u”SAA kumi kamili asubuhi, kikao cha dharura kilikuwa kimeanza eneo la Pugu jijini Dar es Salaam. Mada ilikuwa moja tu; kujadili hatua za kuchukua kutokana na taarifa zilizopatikana usiku kuhusu timu yao maalum waliyoituma Goma kwa kazi maalum.
“Makamanda, bila shaka mmeshtushwa na taarifa kuwa makomandoo wetu watano wako Congo DRC,” alisema Meja Jenerali Obed Mahenda, huku nyuso za makamanda waliokuwa kikaoni hapo zikionesha ubaridi uliotokana na hali halisi kuzunguka suala lenyewe. Hapo akajua kuwa kwanza alikuwa na kazi kubwa ya kuwatuliza wajumbe wale na kuwashawishi wakubaliane na kilichofanyika hadi sasa kabla ya kutaka maoni yao juu ya nini kifanyike zaidi.
“Uamuzi wa kupeleka makomandoo hawa ulifanyika kwa ombi toka ngazi za juu, na ulifanywa na watu wachache sana kwa upande wa ndani, hivyo itanilazimu kuelezea kwa kifupi kwa nini viongozi walituomba sisi kupeleka makomandoo watano, halafu ndipo nitawaeleza kile ambacho inatakiwa tukifanyie uamuzi baada ya taarifa za usiku huu.”
Akazungusha kichwa kuwaangalia wajumbe tisa waliokuwa wamehudhuria kikao hiki. Mmoja kati ya wajumbe hao ni Kapteni Ambrose, rubani aliyekuwa ametumika kuwapeleka wale makomandoo. Watu wote walikuwa kimya kabisa.
“Iko hivi,” aliendelea, “nchi kadhaa zenye mapenzi mema na nchi ya DRC zilifanya kikao cha dharura, hii ilitokana na hali iliyokuwa imejitokeza katika wiki za hivi karibuni, kama mjuavyo kiongozi wa nchi hiyo kwa kushauriana na nchi hizo aliridhia kuitisha uchaguzi mkuu. Pamoja na Tume ya Uchaguzi, Jumatatu wiki ijayo anatarajiwa kutoa tangazo la tarehe ya uchaguzi, kila kitu kilikuwa kimepangwa vyema hadi pale ambapo ICC walipotangaza ghafla kuwa wameamua kumwachia Joseph Katanga siku kumi zilizopita.
Bila shaka wote mlizipata taarifa hizi, Katanga alitumikia kifungo chake cha muda mrefu na sasa alikuwa amebakiza miaka michache ili kumaliza, lakini kwa maelezo kuwa amejutia na kusikitikia vitendo vyake, ICC imeamua kumwacha huru na kumrejesha DRC. Lakini pia, ICC inadai kuwa amebadilika sana kitabia, taarifa hii ilikuwa ya kushangaza na kuchanganya. Kiufundi, kwa muda ulivyo na mazingira, Katanga akishasikia tangazo hili bila shaka atatangaza kugombea. Taarifa za kijasusi zinadai kuwa Katanga ameshaanza kufufua lile kundi lake la waasi na anakusudia kulifanya kuwa chama cha siasa, kurudi kwa Katanga kumeharibu zaidi hali ya usalama huko Goma. Taarifa tulizonazo ni kuwa watu wengi sana wameuawa Goma na kupelekea kuenea kwa magonjwa ya mlipuko eneo hilo hasa kwa vile maiti zimetapakaa mitaani na mvua kubwa bado inaendelea kunyesha, hivyo ili kuweka hali ya usalama na kuhakikisha uchaguzi huu hauingiliwi na Katanga, kazi yetu ikawa ni ‘kumnyamazisha’!
Wenzetu wa DRC hawakutaka kuhusika kwa namna yoyote na huyo Bwana Katanga, hivyo wakaomba msaada, ikiwa kama sehemu ya kutafuta amani ya DRC. Adui wa rafiki yako ni adui yako, na adui wa adui yako ni rafiki yako. Tunaunga mkono serikali halali, ndio maana tumepeleka nguvu yetu kule kukabiliana na waasi, hivyo hii nayo ni sehemu ya kukabiliana na waasi.
Lakini tukiachana na ombi la serikali, mtakumbuka kuwa kwenye mafaili yetu tuna faili lililo wazi dhidi ya mtu huyu, yaani Joseph Katanga. Mnakumbuka ile kashfa ‘Mapandikizi’ ambayo yeye alikuwa mhusika mkuu, hivyo ili kufunga faili lile hatakiwi kuendelea kuishi.
Sasa ni kwamba, makomandoo wanne wamefika salama na tayari wako kwa ajili ya kazi. Ila komandoo wetu mmoja inawezekana akawa amekamatwa na waasi wa Goma, hii ina maana kazi imeongezeka na kuwa kubwa kuliko ilivyotarajiwa. Kazi imekuwa kubwa kwa namna hii; Moja tunatakiwa tuendelee na operesheni yetu ya awali, yaani ‘kumfuta’ Katanga. Pili, inabidi kufanya utaratibu wa kumuokoa komandoo wetu ambaye inaaminika yuko kwenye mikono ya waasi hao ambao wanaongozwa na Joseph Katanga hapohapo Goma. Tatu, ni kufanya uchunguzi wa ndani kujua ilikuwaje parachuti likawa limetoboka kabla ya kutumiwa.
Kwa mujibu wa Kapteni Ambrose ambaye ndiye aliyeongoza ndege na kuwadondosha wale makomandoo kwenye anga ya Goma, komandoo aliyetoweka alilalamika kuhusu parachuti lake kuwa na ubovu, hata kabla hajatoka kwenye ndege, ina maana kulikuwa na parachuti bovu, jambo ambalo si la kawaida, hasa ukizingatia namna utaratibu wetu wa manunuzi ya vifaa vya jeshi ulivyo madhubuti na umakini mkubwa. Haliwezi kuwa kosa tu, siamini kuwa ni bahati mbaya, hivyo nataka kujua undani wa jambo hili kwani inaonesha kuwa mpango wa kukamatwa kwa komandoo wetu ulipangwa tokea hapa. Hiyo itamaanisha kuwa kuna ‘pandikizi’ mwingine wa Katanga, na hii inathibitisha ni jinsi gani mtu huyu alivyo wa hatari sana.”
Meja Jenerali Obed Mahenda alipofika hapo alishusha pumzi ndefu kuashiria kuwa alikuwa amehitimisha maelezo yake ya awali. Hapo ukafuata mjadala mkali sana toka kwa wajumbe wa kikao. Ilipofika saa kumi na moja na robo Meja Jenerali Obed Mahenda alipiga makofi kusitisha mjadala mkali.
“Nikiwasikiliza wajumbe wote naona kimsingi tunakubaliana kufanya haya mambo matatu,” alisema.
“Nimeona watu mmekwenda mbali zaidi namna ya kuyatekeleza, mawazo ya awali yanaonesha kuwa ile timu ya makomandoo walioko Goma igawanywe.
Wawili wamtafute Luteni Pablo Mahene, komandoo wetu aliyetoweka.
Wawili wamtafute Katanga.
Leo ni Ijumaa asubuhi, Tangazo kuhusu uchaguzi linatakiwa kutolewa Jumatatu, ina maana wana saa 72 tu za kukamilisha kazi zote mbili, au niseme tuna saa 72 tu za kufanya kazi hii. Nitawafikishia ujumbe huu ili asubuhi hii ya leo waanze operesheni zao, tunakubaliana hapo?”
Wote waliafiki.
“Sasa kazi ya ndani, mnadhani tufanyeje ili kuchunguza suala hili? Tupate mtu wa ndani au?”
Hapo tena ukazuka mjadala mkubwa sana, wengine wakisema mpelelezi wa ndani hatakuwa huru hasa ikitokea anawachunguza waliomzidi cheo, wengine walisema sheria za ndani haziruhusu mambo kwenda nje.

* * *

Jabir Omari Makame alikuwa jikoni wakati aliposikia simu ya mezani kwake ikilia sebuleni. Si kawaida yake kuamka asubuhi sana na kwenda jikoni, ila kwa ombi la mpenzi wake aitwaye Juliana Owima ilibidi aende jikoni. Mpenzi wake huyo alikuwa mjamzito, ujauzito mkubwa tu, hivyo alimkurupusha asubuhi na kumuomba amtengenezee mayai ya kukaanga.
Hivyo wakati simu ile inaunguruma, yeye alikuwa jikoni. Aliondoka haraka kuelekea sebuleni, hata kabla hajaipokea alishajua kuwa simu ile ingekuwa inatokea ofisini. Ni ofisini pekee ndio humpigia simu ile ya mezani wanapokuwa na hakika kuwa yuko nyumbani, lakini marafiki ndugu na jamaa hutumia zaidi simu ya mkononi.
“Jabir hapa,” alisema baada ya kuweka sikioni kiwambo cha kusikilizia.
“Bila shaka hujambo Jabir, ninakuhitaji haraka iwezekanavyo!” sauti ya mwanamke wa makamo ilisikika.
“Duuh, ofisini siyo?” Jabir Omari Makame aliuliza.
“Hapana, nitakueleza ukiwa njiani unakuja!” ilisema ile sauti ya kike.
“Tuonane hapo ndani ya dakika arobaini zijazo!” Jabir Makame alisema na kuibamiza simu kwenye sahani yake.

* * *
Dakika arobaini baadaye, mpelelezi Jabir Omari Makame alikuwa kwenye gari na Mkurugenzi wa Ofisi Fukuzi, Bi. Anita.
“Kwa mujibu wa Meja Jenerali Obed Mahenda, hali siyo ya kuaminika sana huko ndani, Bi. Anita alisema. “Hivyo hakuona ni salama kama akionana na sisi. Ameridhia kuwa mimi nikuambie kile ambacho nilitaka ukipate toka kwake, nadhani umeelewa picha halisi, swali ni fupi tu, kwa nini yule komandoo alikuwa na parachuti lililotoboka?”
Wakati huo, Bi. Anita alikuwa analizungusha gari kwenye mitaa ya Jiji la Dar es Salaam, hawakuwa na mahali maalum pa kwenda, bali ilikuwa ni njia ya kuhakikisha kikao chao kinamalizikia kwenye gari halafu amrudishe Jabir Makame mahali alipokuwa ameacha gari lake.
Bi. Anita ni mkurugenzi wa kitengo maalum kinachojishughulisha na upelelezi na ujasusi kwa pamoja, hutegemea tu nini kinahitajiwa kwa wakati mwafaka. Kitengo hiki ni cha siri sana na hufahamika na watu wachache sana serikalini. Ni kitengo kilichosheheni vijana makini katika fani hiyo.
“Mbona sioni kama suala hili lina uzito wa kufanya lije kwetu?” Jabir aliuliza.
“Come on Jabir, ni wewe au mimi ninayeweza jua hili ni zito au jepesi kushughulikiwa na ofisi yangu?” Bi. Anita alifoka.
“Okay, suala hili ni zito sana kutokana na kuunganishwa na lile faili liitwalo ‘Pandikizi’. Kuwepo kwa mkongomani Jose Katanga, na ile ishu ya kupandikiza watu aliyoifanya kunafanya iwe ni kazi inayotakiwa kufanyika kwa umakini na kupewa uzito mkubwa sana!” Bi. Anita alisema.
Halafu akaongeza, “Hili faili lina taarifa zote namna hayo maparachuti yalivyonunuliwa hadi kukabidhiwa kwa Kapteni Ambrose ili yatumiwe na wale makomandoo watano. Jabir, una saa zisizozidi sabini na mbili kuleta ufumbuzi wa suala hili, mpango ni kuwa Rais wa Congo aendelee na mpango wa kutangaza siku ya uchaguzi. Fanya kila unaloweza ukweli upatikane ndani ya muda huo. Hiki hapa ni kibali maalum ambacho kinakuwezesha kufanya mambo ambayo katika hali ya kawaida usingeyafanya hasa kwa sababu ya aina ya watu unaoweza kukabiliana nao katika kazi hii!”
Akazungusha usukani kushika barabara ambayo inaelekea Upanga, sehemu ambayo walikuwa wameliacha gari la mpelelezi Jabir Omari Makame. Jabir alilichomeka lile faili kwenye koti lake.
Ilikuwa inagonga saa kumi na mbili na dakika arobaini na tano asubuhi wakati Jabir alipotoka kwenye gari la Bi. Anita kwenda kwenye gari lake.


* * *

Wakati mpelelezi Jabir Makame akiwa anaingia kwenye gari lake, ni wakati huohuo hawa walikuwa kwenye maongezi kwa simu.
“Kama yeye ndiye amepewa kazi ya kupeleleza kisa hiki basi nakupa saa ishirini na nne kuhakikisha kuwa Jabir anakuwa Kinshasa!” Sauti ya Joseph Katanga ilisema kwenye simu.
2


K u m e p a m b a z u k a n a H e s a b u Z a k e
ALIPOWASILI nyumbani kwake maeneo ya Makongo Juu, tayari ilikuwa saa moja na dakika tatu asubuhi. Ukweli ni kuwa, pamoja na kuelezwa na kusisitizwa na Bi. Anita, lakini bado mpelelezi Jabir hakuwa ameipa uzito mkubwa ile kazi aliyokuwa amepewa, aliona kuwa walikuwa wanajiingiza kufanya kazi za kihisia zaidi, alishindwa kumkatalia bosi wake. Alipofika nyumbani kwake alipitiliza chumbani ambako alimkuta mpenzi wake akiwa bado amelala.
“Vipi Jabir?” Juliana alimuuliza kama aliyekuwa akitarajia habari fulani.
Tangu amjue Jabir, sasa huu mwaka wa tatu, japo hawajaoana, lakini wamekuwa wakiishi kama mke na mume. Alishajua kuwa simu ikipigwa kwa ile simu ya mezani basi itakuwa inatokea ofisini. Pia kwa kuzingatia muda ambao simu hiyo imepigwa, ilikuwa wazi kuwa kulikuwa na jambo la muhimu sana, ndio maana mpigaji alishindwa kusubiri Jabir aende kazini muda wa kawaida wa kazi.
“Safi, kuna kazi tu kidogo!” Jabir alisema.
“Hausafiri?”
“Hapana, nipo hapahapa, ni kazi za ndani tu!” Jabir alisema huku akibwaga lile faili kwenye meza ndogo iliyokuwa pembeni mwa kitanda. Akambusu Juliana halafu akasimama akiwa anavua shati.
“Umependa mayai niliyokuandalia?” Jabir alimuuliza wakati akielekea bafuni.
“Ndiyo, asante!” Julian alisema kwa sauti ya chini kiasi.
_________________


Saa 1:30, Goma DRC

Meja Kabananga, maofisa wengine wa jeshi pamoja na wale makomandoo wanne walikuwa kwenye kikao kizito, ilikuwa kikao cha mkakati wa operesheni maalum.
“Ngome kuu ya hawa waasi iko hii sehemu ambayo wao wameibatiza jina Bunagana a.k.a Paradiso ya Jose Katanga,” Meja Kabananga aliwaambia wanakikao wenzake. “Iko eneo la mpakani kati ya Congo na Rwanda, kambi hii ilijengwa na Wabelgiji wakati wakiwa wanatawala iliyokuwa Zaire, tumeshafanya mashambulio mara kadhaa kwa miaka mingi lakini imekuwa ngumu sana kuwamaliza kabisa waasi hawa maana wengi wao hukimbilia Rwanda pale wanapoona mashambulizi yamekuwa magumu.
“Hivyo basi, njia pekee iliyobaki kuwamaliza waasi hawa ni kuua viongozi wao wote waandamizi. Hilo nalo limekuwa gumu sana maana imekuwa ngumu sana kuwapata wote na wamekuwa wakitumia majina na sura za bandia, ila vyanzo vyetu vya habari vinasema Jose Katanga kaitisha kikao cha siri ambapo makundi mbalimbali ya waasi wa Congo yanatarajiwa kukutana eneo hilo liitwalo Bunagana a.k.a Paradiso ya Jose Katanga. Viongozi wanaotarajiwa kuhudhuria ni hawa hapa.”
Akaweka picha zipatazo kumi na moja kwenye meza ya duara ambayo wajumbe wa kikao hicho walikuwa wamekaa kuizunguka, wajumbe walianza kuziangalia zile picha. Mwishoni zilibaki kwenye mikono ya wale makomandoo wanne.
“Hapa ndio Bunagana a.k.a Paradiso ya Jose Katanga,” Meja Kabananga alisema huku akiwa amesimama na kuonesha ramani ya eneo hilo lililo Mashariki mwa Kivu kaskazini. “Inadhaniwa kuwa eneo hili kuna handaki kubwa sana limejengwa hapa kwenye hili jengo linaloitwa THE ROCK. Ni ndani ya jengo hili liitwalo The Rock ndipo inadhaniwa kuwa Joseph Katanga hupenda kukaa. Wengi wamejaribu kwenda hapa lakini imeshindikana, na sababu kuu ya kushindikana ni jinsi ambavyo kimahesabu inakuwa ngumu sana. Unaona hivi vilima sita ambavyo viko pembezoni mwa kambi hii? Kutoka kwenye kila kilima kwenda ilipo The Rock ni mita 500, juu ya kila kilima inaaminika kuwa kuna wadunguaji wasiopungua watatu ambao wana kazi kuu tatu. Mdunguaji mmoja wa kila kilima huwa ana kazi ya kumuangalia Joseph Katanga. Hivyo ikitokea jambo lolote la kuhatarisha maisha yake, risasi ya mdunguaji huyo huchukua maisha ya chochote ambacho kinahatarisha maisha ya bwana wao huyo wa vita. Nadhani mnaelewa naposema wadunguaji, yaani, snipers! Bunduki zao za kisasa zenye darubini za kisasa zinauwezo mkubwa wa kuona mbali na kuchukua shabaha ya mbali. Hii ina maana wadunguaji sita wako macho muda wote kumuangalia Katanga.
Mdunguaji wa pili aliyeko kwenye kila kilima, hii inamaana wadunguaji sita, wao kazi yao ni kufuatilia milango mitatu ya kuingilia kambi hiyo na kufuatilia wageni wote. Hivyo unapokuwa mgeni jua kuwa kuna mdunguaji anakufuatilia kwa mbali.
Mdunguaji wa tatu aliyeko kwenye kila kilima huwa hana kazi maalum. Hivyo yeye huwa tayari kwa dharula yoyote itakayojitokeza. Lengo ni kuona kuwa wale wadunguaji wawili wa awali hawaachi kufanya kazi zao muhimu.
Katanga siyo mtu wa ratiba maalum, inadhaniwa kuwa ana marafiki wachache sana anaowaamini, marafiki hao hawajulikani hadi sasa. Katanga ni mtu aliyekamilika katika kutumia silaha yoyote, ana uwezo wa juu katika kutumia mwili wake kujikinga na kushambulia. Anaogopwa na kupendwa sana na watu wake hasa jamii ya wakulima ya kabila la Lendu, inadhaniwa kuwa wazee walioko vijiji vya jirani hupewa zawadi na vitu mbalimbali na Katanga ili wawe wanampa taarifa yoyote ambayo wanadhani ni hatari kwake.

Njia pekee ya kwenda huku ni hii hapa, lakini njia hii inalindwa kuliko kitu chochote kile. Upande huu kuna ziwa na upande huu kuna mpaka na Rwanda ambapo jeshi la nchi hiyo lina kituo chake kikubwa eneo hili…” alizidi kufafanua Meja Kabananga.
“Kamanda, tumeshafanya upembuzi wa kutosha kabla ya kuja hapa, na njia pekee ambayo tunaweza kufanikisha misheni hii ni kwa sisi kukamatwa halafu tutajua cha kufanya tukishafika huko. Hakuna namna nyingine ya kuingia na kuwafanya kitu mbaya bila siye kuwa mateka kwanza!” alisema Kamanda Twaha Mchopa ambaye licha ya kuwa komandoo pia ni mtaalamu sana kwenye mambo ya mikakati.
“Sawa, sasa mtafanikishaje hilo maana mtu anaweza kuamua kukuua badala ya kukuteka? Tutahakikishaje kuwa mnatekwa badala ya kuuawa?” afisa mwingine wa Jeshi la Congo alihoji.
“Hilo tuachieni sisi! Kwa sasa tunahitaji saa nne za kujiandaa. Mbili za kulala halafu mbili nyingine za kupanga mkakati na kuondoka hapa!” alisema Musa Buti huku akiwaangalia wenzie wanne.
“Mtahitaji gari ili liandaliwe?” alihoji Meja Kabananga ambaye alishajua kuwa alikuwa akiongea na makomandoo hivyo kuuliza maswali madogomadogo lisingekuwa tatizo.
“Ndiyo, nimesikia wale waasi wanatumia Spartan 4 x 4, je, mnazo aina hiyo?” Musa alihoji.
“Tunazo, hata walizonazo walipora kwetu,” alijibu meja Kabananga.
“Tunaihitaji hiyo, iwe tayari muda wowote kuanzia sasa!” Musa Buti alisema.
“Halafu chumba mlichonipa kuna shida, kuna bomba linadondosha matone ya maji, kutokana na aina ya ile sakafu yale matone yanakuwa kama yanadondokea kwenye sufuria tupu, imenifanya nisilale vema. Huu muda wa kuikusanya akili na utayari wa kifikra kwa kazi ngumu iliyoko mbele yetu nitahitaji suala hilo lishughulikiwe. Sitaki ule mlio!” Mark Muga mmoja wa wale makomandoo, alisema.
“Nitatafuta fundi mwingine, maana fundi wetu wa kawaida alikutwa ameuawa usiku wa kuamkia jana,” alisema Meja Jean Francis Kabananga.
“Ameuawa hapahapa kambini?” alihoji kamanda Emily Otieno, mmoja wa wale makomandoo ambaye alikuwa kimya muda mrefu. Kwa asili yeye ni mkimya sana.
“Ndiyo, inaaminika ameuawa na mmoja wetu kwa sababu ya wivu wa mapenzi, wajua tuna wanawake sita tu hapa kambini na tuko wanaume zaidi ya mia na hamsini. Nadhani unaweza kuelewa hali hii,” alisema Meja Jean Francis Kabananga.
“Ukata! Hahahaha!” kamanda Musa Buti alisema huku akichukua ile ramani ambayo Kabananga alikuwa akiitumia kuwaelekeza juu ya Bunagana a.k.a Paradiso ya Jose Katanga, akimkabidhi Mark Muga.

* * *

Saa mbili za kwanza za mapumziko, wote walikuwa kwenye vyumba vyao vidogo sana vilivyokuwa kwenye moja ya majengo yaliyokuwa kwenye kambi hiyo, Kambi hiyo ilizungukwa na msitu mnene. Vyumba hivyo vilikuwa na giza sana, halafu kwa sababu za kiusalama hakukuwa na milango kwenda vyumbani. Hapakutofautiana na pango. Kuta nene sana, imara, vitanda vya mbao tu hakuna godoro, taa hafifu sana kiasi ulihitaji kuwa na uono mzuri kuweza kumuona mtu, vilikuwa maalum kwa ajili ya mapumziko. Kulikuwa na choo ndani ya kila chumba na bomba la maji pembeni yake. Ni bomba hilo ambalo walikuwa wamelilalamikia.
Tayari zilipita dakika ishirini tangu pale walipopeana saa mbili za kupumzika na kukusanya akili zao pamoja. Inaaminika kuwa makomandoo kabla hawajaanza operesheni ngumu huhitaji muda kama huo kwa ajili ya zile sala zao na kuweka akili na hisia katika kiwango kinachotakiwa, kwa hivyo hutumia muda huo kwa ajili ya kutafakari.
‘Ta’
‘Taa’
‘Taaa’
‘Taaaa’
“Mxccchyuuuuuu’ Emily Otieno alisonya kutokana na kero iliyoletwa na mlio huo wa matone ya maji yaliyokuwa yakidondoka sakafuni. Alisimama akaenda kujaribu kulifunga tena lile bomba, lakini hakufanikiwa, akaamua kuukaribisha ule mlio kwenye ubongo wake na kuupa nafasi kisha afanye alichotaka. Akafanikiwa. Mlio uliendelea kuwepo lakini hakuuona kama kero tena kwa vile alishaukubali na kuupa nafasi kwenye mfumo wake wa kufikiri.
Saa moja ilipopita wote walikuwa wamezama kabisa kwenye fikra zao huku wakijaribu kutembea kifikra. Wakifikiria kila aina ya hatari ambayo wanaweza kukutana nayo, wakati huohuo walitumia fikra zao kujikumbusha uwezo wao na jinsi walivyo wa kipekee. Kila mmoja alijiambia kuwa ilikuwa kazi ya hatari sana waliyokuwa wakienda kuifanya, lakini wakajikumbusha kuwa ndio maana walipewa mafunzo ili kufanya kazi ya hatari iwe sehemu ya maisha yao.
Kila mmoja alikuwa kwenye chumba chake. Vyumba vyao havikuwa karibu kwa sababu maalum pia. Komandoo Muga alikuwa kitandani amelala chali huku macho yamefumbwa. Komandoo Otieno alikuwa amelalia ubavu wa kulia huku uso unatazama ukuta. Komandoo Mchopa alikuwa ametumbua macho, akiliangalia lile bomba lililokuwa likidondosha maji. Japo macho yalikuwa wazi, yamemtoka, lakini hayakuwa timamu kwani akili ilikuwa kwingine.
‘Ta’
‘Taa’
‘Taaati’
‘Taaaatii’
Ni Twaha Mchopa peke yake aliyeweza kuhisi utofauti kwenye mlio huo wa matone. Ile ‘ti’ ya mwisho ilimrejeshea umakini kuelekea kwenye lile bomba. Macho yakarejeshewa mawasiliano, japo hakujitingisha lakini ilimshangaza, kama kila kitu kiko kama ilivyokuwa awali kwa nini mlio umebadilika japo ilikuwa mabadiliko madogo sana.
Ilipopiga ‘taaaati’ nyingine ndipo macho yake yalipobaini kuwa ile ‘ti’ ilikuja na muonekano wa buti ya jeshi iliyokuwa imejitokeza kwenye ukuta mmoja wa mlango kwa nje! Aliangalia eneo lile, alikuwa na hakika kuna mtu alikuwa amenyata hadi kufika pale, na sasa akajua nini kilikuwa kinafuata, yule mtu alikuwa anasubiri tone jingine ili tena apige hatua nyingine na kusababisha ‘ti’ nyingine ambayo ingemfikisha mtu huyo katikati ya ule mlango.
Komandoo Twaha Mchopa hakufanya purukushani, alichomoa kisu toka kwenye buti yake. Kitendo hicho alikifanya kwa namna ambayo hata angekuwa mgongoni kwako usingesikia, sasa akawa anasubiri tone lije.
Ghafla akaona mguu uko hewani unasogezwa katikati ya mlango. Hii ikamjulisha kuwa mtu aliyekuwa hapo alikuwa ameshasoma muda uliotumika kati ya tone moja hadi jingine, hivyo alinyanyua mguu akiwa anasubiri ashushe pamoja na tone la maji! Kitendo hiki kilimshangaza sana Twaha Mchopa, hakuwa amefikiri kuwa maji yale yalikuwa yamefanywa vile kwa kusudi ili mtu akinyata asisikiwe. Akawa tayari anasubiri na kisu chake. Swali moja likawa kichwani mwake ni; kama wenzie watakuwa wamebaini hila hiyo.
“T..” Hakusubiri ule mlio uishe, kama umeme alirusha kisu ambacho wakati kinafika usawa wa ule mlango kilikutana na kifua cha mtu ambaye ndio kwanza alikuwa anatua mguu wake ili kukamilisha ile ‘ti’. Jamaa alianguka kama gunia huku kisu kikiwa kimezama kwenye titi lake la kushoto. Alikuwa amevaa sare za jeshi. Jeshi la Congo. Ilimshangaza, mara moja akajua ilimaanisha nini, hakutaka kupoteza muda. Alimvutia ndani yule mtu, akamvua sare zake na kuzivaa yeye.
Akakwapua begi lake na vifaa muhimu, akatoka kwenye kile chumba. Alipofika chumba cha Muga, alipiga mguu wake chini mara mbili halafu akasubiri kidogo. Hiyo ndio ishara waliyokuwa wamepeana ili kuepusha hatari iwapo mmojawao angetaka kwenda kwa mwingine bila tarifa. Aliposimama mbele ya mlango alipigwa na butwaa. Muga alikuwa kitandani huku akiwa na matundu matatu ya risasi kichwani. Hakutaka kupoteza muda alishajua kuwa mwenzie alikuwa ameshawahiwa, hivyo alivamia begi la Muga akachukua vitu kadhaa ikiwepo ile ramani ya kuelekea Bunagana a.k.a Paradiso ya Jose Katanga.
Alipofika mlangoni wakati anataka kutoka, mara akakumbuka kitu. Akaangaza macho pale sakafuni, akaona alichokuwa akikitafuta; ganda la risasi. Mwanga ulikuwa hafifu sana, hivyo akalifutika mfukoni. Sasa akaazimia kwenda kuwaona wenzie wengine ili kuwapasha habari. Alipopiga hatua ya tatu mara akasikia mlio wa king’ora cha kuashiria kuwa kulikuwa na hatari.
“Shit!” Twaha Mchopa alisema kwa hamaki, ilikuwa inatimia saa nne na nusu asubuhi wakati hali hii ikitokea. Hali ilikuwa ya giza kubwa nje kutokana na wingu na mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha.
* * *

Saa nne na nusu hiyohiyo wakati Komandoo Twaha Mchoppa akihamaki ndani ya ile kambi ya jeshi ndani ya msitu uliko Goma, yeye mpelelezi Jabir Omari Makame alikuwa kitini akisubiri kuonana na mwakilishi mkuu wa kampuni ya China Army Cargo.
Kwa mujibu wa nyaraka alizokuwa amepewa na Bi. Anita ambaye alikuwa amepewa na Meja Jenerali Obed Mahenda, kampuni hiyo ndio iliyouza vifaa mbalimbali ambavyo vilijumuisha ile Parachuti iliyoharibika na kusababisha kutekwa nyara kwa yule komandoo mmoja aitwaye Pablo Mahene. Aliona ni sehemu nzuri ya kuanzia upelelezi wake huo ambao hakuwa ameupa uzito wowote.
“Eti kaka ulikuwa umeweka miadi ya kuonana naye?” alihoji msichana aliyekuwa mapokezi ya ofisi hiyo ndogo tu, Jabir Omari Makame alikadiria kuwa ofisi hiyo ilikuwa na watu kati ya sita na kumi, ilionesha wazi kuwa haikuwa ofisi ya kuhifadhi vitu bali ya kukusanya taarifa, kuonana na wateja halafu kuwasiliana na ofisi yao kuu iliyoko China kwa ajili ya hatua za mbele za kibishara. Hivyo haikuwa ofisi kubwa, pengine ndio maana mkuu wa ofisi hii aliitwa Mwakilishi Mkuu wa kampuni yaani ‘Country Representative’.
“Hapana, kwani ni lazima kila anayekuja awe amefanya miadi naye?” Jabir alihoji.
“Hapana, ila nimeuliza kwa vile inaonesha kuwa hakuwa na taarifa za ujio wako na ndio maana hayupo ofisini muda huu,” alisema yule dada wa mapokezi, ambaye alikuwa na sifa zote kiumbile kuwa kwenye nafasi hiyo.
“Nilipata moyo sana nilipoona gari yake iko hapo nje hivyo nikajua yupo,” Jabir alisema.
“Gari ipi?” yule dada aliuliza kwa kubabaika kidogo japo alijitahidi kuficha hali ile.
“Hiyo hapo nje!” Jabir alijibu huku macho yake yakiwa makini kuusoma uso wa yule dada.
“Aaah ni kweli, lakini huwa anaiacha hapo hiyo gari inapofika weekend kwa vile mara nyingi hupenda kutumia muda huu nje ya Dar es Salaam,” alisema yule dada kwa sauti ya kujiamini lakini ambayo hakuweza kumficha Jabir kuwa alikuwa amedanganywa.
“Sawa, sasa lini tena naweza kumuona?”
“Unatokea kampuni gani umesema!?” yule dada alimuuliza huku akishusha pumzi.
“Papaso Security!” Jabir alisema huku akimpatia kadi ya biashara.
“Okay, nitajitahidi kukuwekea miadi halafu nitakutaarifu,” alisema yule dada huku akiwa anasoma taarifa zilizoko kwenye ile kadi ya biashara.
“Nitashukuru sana, sikumbuki kama umeshaniambia unaitwa nani?” Jabir alisema na kuuliza.
“Hapana, naitwa Omega!” alijibu yule dada.
“Omega tu?!”
“Omega Odemba!” dada huyo alisema huku akimuangalia Jabir kwa macho yake yenye kuvuta.
“Okay, Omega. Nitasubiri simu yako maana nahitaji sana kuonana naye!”
“Hamna shida, ni vile tu umekataa kuniambia maana ningeshamwambia shida yako, labda hadi siku mnaonana angekuwa ameshakuandalia majibu ya kile unachohitaji!” Omega alisema.
3


T u k u t a n e G o m a D R C


JABIR Makame hakwenda mbali toka ofisi hiyo, alishaona dalili njema. Majibu ya Omega na jinsi alivyokuwa akibabaika vilimwambia asiondoke hapo. Kama mpelelezi kazi yake ni kutafuta mwanya, ama waweza sema kutafuta harufu ama manukato inategemea tu kile anachotafuta. Aliiona hiyo kwenye macho ya Omega, midomo yake ilivyomcheza kusema uongo, mashavu yake yalivyovutika kutengeneza tabasamu la uongo.
Hivyo, dakika kumi baadaye aliegesha gari tofauti na lile lake umbali kidogo toka zilipokuwa ofisi za China Army Cargo zilizoko Mtaa wa Lumumba. Makadirio yake ilikuwa ni kwamba kama mtu aliyetaka kuonana naye angekuwa yupo ofisini, bila shaka angetoka wakati wa chakula cha mchana kwenda kula.
Makadirio na kutabiri matendo na matukio ni sehemu ya kazi ya upelelezi. Aliangalia saa yake. Ilikuwa saa sita na nusu, hivyo akakadiria kuwa ikifika saa saba bila shaka mtu wake angekwenda kupata chakula cha mchana. Akajiegemeza kwenye kiti huku macho yakiwa makini kuangalia ile ofisi.
Ilipofika saa saba kasoro dakika ishirini mara akaiona Nissan ya rangi ya bluu ikiwasha taa kuashiria kuwa ilikuwa ikiingia sehemu ya kuegesha magari ya China Army Cargo. Akawa makini kuangalia gari lile. Walishuka watu wawili waliotembea haraka kuingia ndani ya ofisi. Dereva alibaki kwenye usukani.
Baada ya dakika tano, alitoka mtu mmoja na kuingia ndani ya ile Nissan. Ikaondoka. Hii ina maana mtu mmoja alibaki ndani, Jabir Makame akakadiria kuwa labda yule mtu ni mfanyakazi wa kampuni hiyo au ni mteja. Aliiangalia Nissan ile ikipotelea mbele ya macho yake, akaendelea kujiegemeza kwenye kiti akisubiri muda aliotarajia kuona kitu.
Kweli ilipofika saa saba kasoro dakika tano, macho yake yaliwaona watu wawili wakiwa wanatoka ndani ya jengo lile, wa mbele alionekana ni mtu mzima aliyenawiri na mwenye uso wa neema. Aliangaza macho huku na huko kama anayekagua, halafu aliweza kumtambua mtu aliyekuwa nyuma yake. Alikuwa ni yule mtu aliyekuwa amekuja na ile Nissan, yule mtu aliyenawiri alikwenda upande wa dereva wa ile Toyota Land Cruiser V8 halafu yule mtu aliyekuwa amekuja na Nissan alipanda upande wa nyuma. Gari likaondolewa taratibu sana.
Jabir aliliangalia kwa makini, halafu alipojiridhisha kuwa lilikuwa limefika umbali wa kutosha na yeye akaliingiza gari lake barabarani, akaanza kuifuata ile V8. Kutoka Lumumba akakata kushoto na kuingia Barabara ya Uhuru mara tu baada ya kuimaliza Hospitali ya Mnazi Mmoja, wakanyoosha na hii barabara hadi walipofika mnara wa saa, wakakata kushoto.
Hapo mbele wakawasha taa kuashiria kuwa wanaingia PX Delux. Mara moja Jabir akajua kuwa walikuwa wanakwenda hapo kwa ajili ya chakula cha mchana, alipitiliza na kuwaacha wao wakiwa wanaelekezwa na mlinzi namna ya kuegesha gari. Akanyoosha na hiyo Barabara ya India hadi alipofika Mtaa wa Zanaki, halafu akaingia kulia kwenye Barabara ya Samora, akaanza kurudi alikotoka japo ilikuwa mtaa wa pili.
Saa saba na dakika tano, mpelelezi Jabir Makame alikuwa akichungulia kwa makini sehemu ambayo kulikuwa na watu wamekaa wakipata chakula cha mchana. Kwa vile alikuwa ameingilia upande wa nyuma na kutokea ilipo sehemu ya msalani, alikuwa amepewa mgongo na wengi wa watu. Hakupata shida kumuona yule mtu aliyenawiri akiwa na sahani pembezoni mwa meza ndefu ya chakula cha kujihudumia akingoja zamu yake ifike.
Kulikuwa na watu wanne mbele yake. Ilikuwa ni sehemu iliyojaa watu wazito, huhitaji elimu kubwa kuliona hilo. Macho yao, matendo yao, namna walivyopakua chakula, namna walivyokula, namna walivyoongea, aina ya muziki na mandhari yote kwa ujumla, vilithibitisha hilo.
Jabir hakutaka kupoteza muda mwingi hapo, alitaka kuongea na yule bwana. Aliangaza na kuangalia uwezekano wa yeye kuongea naye, alipozungusha macho hatimaye alimuona yule mtu aliyekuwa ameletwa na Nissan ya bluu, kwa jinsi alivyosimama na alivyokuwa akiangalia, mara moja Jabir akajua yule mtu alikuwa ni mlinzi. Okay, amepewa mlinzi binafsi!! Na nani? Kwa nini? Wangekuwa na duka la silaha sawa lakini kwa kazi ya kuunganisha wateja na ofisi zao China?! Maswali ya mshangao yakafumuka kichwani kwa Jabir. Hata hivyo, alidhamiria kumchukua mtu wake! Wakati anafikiria hilo, mara akamuona yule jamaa aliyeonekana kama mlinzi wa yule aliyenawiri akiwa anakuja upande huu aliokuwepo.
Ameniona nini? Jabir alijiuliza huku akijiweka sawa, Jamaa sasa akawa anakaribia kabisa eneo hili la vyooni, Jabir akajiweka tayari kwa lolote. Alipiga hatua chache hadi ulipokuwa mmoja wa milango ya choo, akawa kama anayefungua. Wakati huo yule jamaa alipita na kwenda mlango uliofuata, akafungua na kuingia, kabla hajafunga mlango, alishangaa mlango unasukumwa.
“Kuna mt…” kabla hata hajamaliza kusema, alipokea ngumi kali sana ya uso, halafu kitambaa kikatua puani kwake, alipohema tu, usingizi mzito ukamchukua. Jabir alimkalisha kwenye sehemu ya kukalia ya choo, akawa kama mtu anayejisaidia. Haraka sana Jabir aliingia kwenye choo kingine akatupa kile kitambaa na ku-flash maji. Halafu akawahi sehemu yenye maji, akanawa mikono yake. Alirudi sehemu ambayo watu walikuwa wakichukua chakula. Akamuona mtu wake akiwa ameshakaa mezani, bahati ilikuwa upande wa Jabir kwa vile mtu huyu alikuwa kwenye meza ya peke yake. Hivyo alimfuata.
“Habari yako mheshimiwa!” Jabir alimsalimia, Jamaa alipomuona Jabir alishtuka nusura haja ndogo imtoke. Mshtuko huo ulimwashiria Jabir kuwa mtu huyo alikuwa anamfahamu na alikuwa na taarifa zake.
“Nataka kuongea nawe!” Jabir alisema huku akimuashiria yule jamaa asimame.
Akatii na kusimama.
“Tangulia!” Jabir alimwamuru.
Kwa uzoefu wake alishagundua kuwa mtu huyu hakuwa mzoefu wa haya mambo. Walitembea hivyo kistaarabu hadi walipofika mahali ambapo Jabir alikuwa ameegesha gari lake. “Ingia ndani!” aliamrisha tena baada ya kuwa ameshafungua mlango wa gari.
“Unanipeleka wapi wewe? Unajua unajisumbua? Huwezi kushindana na hawa watu!” yule jamaa alisema.
“Kina nani?”
“Kwani wewe unamtafuta nani?” Jamaa naye aliuliza wakati Jabir akiwa amewasha gari.
Wakati huo Jabir alikuwa amemfunga pingu za mikono na miguu na pingu hizo kuunganishwa kwenye chuma maalum kwenye kiti cha nyuma. Akaliondoa gari taratibu. Askari wa eneo hilo la kuegesha magari la hoteli hiyo alimwondolea kizuizi cha chuma huku akimuonyeshea mkono wa kuomba chochote. Jabir alikunja kushoto na kuliondoa gari kwa kasi.
“Nawatafuta hao uliosema siwezi kushindana nao!” hatimaye Jabir alimjibu huyo jamaa.
“Nimeshakuambia huwawezi!” alisema yule jamaa.
“Unaitwa Sadick Joseph siyo?”
“Ndiyo, umejuaje?”
“Unaishi Kunduchi namba 0071 siyo?”
“Umejuaje haya yote? Wewe si umeanza kazi asubuhi hii?”
“Mkeo anafanya kazi mafao, tena sasa hivi bado saa mbili atoke kazini siyo? Mwanao wa pekee yuko IST, na unajua kabisa huna uwezo wa kuzaa tena si ndiyo!?”
“Shiiiit how do you know all this?” Jamaa alibaha.
“Jibu swali langu, nani yuko nyuma ya mpango huu?” Jabir alimuuliza huku akiwa anashika njia ya kwenda Mbagala.
Jamaa alionekana kuchanganyikiwa sana. Hata hivyo alijifanya kichwa ngumu.
“Mpango gani?”
“Sasa nitawaambia wanaotaka kumchukua mwanao wafanye hivyo kama hutoniambia, halafu mkeo naye utampoteza!” Jabir alisema pasi masihara.
“Nimeshaharibu maisha yao, kwa sababu hata nikikuambia, bado watawaua mwanangu na mke wangu, hakuna namna naweza waokoa sasa…Oooh shit” Jamaa aliongea kwa jazba na sauti ya juu.
“Nitajie mmoja tu!” Jabir alizidi kusisitiza.
“Kwa kweli mimi sijui, ila nimepigiwa simu asubuhi hii nikaambiwa utakuja kunihoji. Sijui zaidi ya hilo!” Alilalamika yule jamaa.
“Nani aliyekupigia simu?”
“Alijitambulisha kwa jina la KK.”
“Yuko wapi?”
Kimya.
“Unajua wewe unafanya mzaha, nauliza huyo aliyekupigia nitampata wapi?”
Kimya.
“Hutaki kusema?”
Kimya.
Jabir akachungulia kwenye kioo cha mbele cha kuonea nyuma, akamuona abiria wake akiwa ametulia. Akapunguza mwendo wa gari, akageuka kumuangalia. Alikuwa amelala huku povu jeupe likiwa limemjaa mdomoni.
“Cynide Pill” Jabir alinong’ona. Alishajua kuwa yule mtu alikuwa ameamua kujiua kwa kutumia vidonge viitwavyo Cynide. Hakutaka kupoteza muda, alitafuta mahali pa kugeuza gari na akaligeuza. Maswali mawili yakawa kichwani, nani alimpigia simu Sadick? Pili kwa nini waliamua kufanya biashara na kampuni ya namna hii?
Alipata sehemu ya kugeuzia gari, lakini kabla ya kuingia barabarani, alichukua simu yake ya mkononi kisha akaanza kutafuta vitu fulani kwenye mitandao. Baada ya dakika kumi hivi akawa amepata namba kadhaa.
“Phil unaweza niangalizia simu zilizoingia kwenye namba hizi za simu asubuhi ya leo?” Jabir alisema, halafu akakata simu. Aliliingiza gari barabarani. Aliendesha taratibu tofauti na alivyokuwa akija, baada ya muda simu yake ya kiganjani iliita.
“Sema Phil!” Jabir alisema halafu akasikiliza.
“Shiiiit, haiwezekani, itakuwaje toka nyumbani kwangu aisee!!? Na sauti je?” sasa Jabir alihamaki.
“Come on Phil. bullshit! Imepigwa muda gani?” alihoji huku sasa akilichochea gari kwa kasi.
“Phil hebu niambie muda ambao simu hiyo ilipigwa!” Jabir alisema kwa sauti ya taharuki.
Akasikiliza kidogo kisha akabwata: “Mmmmh, saa tatu na nusu! Ina maana saa nzima tangu nitoke nyumbani!” Halafu akatukana tusi kubwa sana na kukata ile simu.
Aliangalia saa yake tayari ilikuwa imetimia saa nane mchana. Sasa akili yake ikawa nyumbani kwake ambapo kumbukumbu ya mwisho alimwacha Juliana mpenzi wake akiwa bado yuko kitandani amelala.
Gari lilipanda ule mlima wa Makongo Juu kwa kasi ya ajabu. Alipofika nyumbani kwake alikimbilia ndani, alipofika mlangoni tu akapokewa na matone matatu ya damu. Akachanganyikiwa. Akakimbilia chumbani kwake. Huko akapokelewa na chumba kilichovurugwa sana, akajikuta amesimama asijue cha kufanya. Haraka akajaribu kumpigia simu Juliana. Simu ilipokelewa!
“Hili ni tangazo la mwisho kwa abiria Juliana Owima, Khalid Katanga na Kakengo Diomo wanaosafiri kwa Shirika la Ndege la South African Airways, kuwa waingie ndani ya ndege tayari kwa safari!”
Halafu simu ikakatwa. Jabir akajaribu kupiga tena na tena ikawa ndio mwisho wa kuipata ile simu. Alitamani aruke awe uwanja wa ndege ili kuzuia. Akajua hilo lisingewezekana. Alitamani afanye kitu lakini hakujua kitu hicho ni kipi. Alijiona wa ajabu sana kama angeshindwa kumsaidia mpenzi wake.
“Watu hawa wanaharamu sana, naapa nitafanya kila niwezalo niwapate!” alisema huku macho yakiwa yamemuiva na machozi yakimlengalenga. Akajikuta ameweka kila mpango kando na sasa akili yake ikawa kumfuata Juliana na kumuokoa. Alichukua vitu muhimu kwa ajili ya kusafiria, akaweka sawa kila kitu akawa tayari kwa kuondoka.
Aliiangalia nyumba yake kama anayeiaga kwa kuwa alikuwa anakwenda safari asiyoijua mwisho wake. Alipofika kwenye gari ndipo alipokumbuka kuwa alikuwa na maiti ya Sadick Joseph, halafu akakumbuka maneno ya Sadick Joseph “Unajisumbua bure watu hawa hutowaweza”.
“Nitawaweza!” alifoka huku akiibeba ile maiti hadi sebuleni kwake. Akaiacha hapo na kuufunga mlango tena. Alikuwa na hakika kuwa lazima watu toka ofisini kwao wangekuja kufanya uchunguzi wa kilichotokea, ni watu hao ambao wangeishughulikia ile maiti.
Safari hii hakuwa kwenye umakini wake. Aliliondoa gari kwa namna ambayo mbwa wa jirani wakaanza kubweka na kuku wakaanza kupiga kelele kufuatia mlio wa injini na matairi yalivyojiburuza, sasa alikuwa akielekea uwanja wa ndege! Gari liliendeshwa kwa fujo sana hata wakati simu ya Bi. Anita, mkurugenzi wa Ofisi Fukuzi inaingia aliiona kama kero, hata hivyo aliipokea.
“Hello, Jabir! Nimepata taarifa zako kupitia Phil. pia tumeweza kusikia simu yako ya mwisho na mchumba wako, tuko pamoja na wewe, najua siyo rahisi kwa sasa kukuzuia usisafiri, naelewa ila kuwa makini sana!” Bi. Anita alisema kisha akakata simu. Hakutegemea kupata majibu ya Jabir.
Wakati anaweka simu chini akasikia ujumbe umeingia, akaupuuza. Alipita Ubungo kwa namna ambayo pikipiki ya polisi wa bararani ikaanza kumfukuza, hakujali, akazidi kuliburuta lile gari. Alipofika mbele ya external hakutaka kuendelea na kupitia Tazara, hivyo akaingia kulia ili apitie Vingunguti Mahakama ya Mbuzi, huku pikipiki ya polisi ikiwa bado inamuandama, aliendelea kuiburuta gari. Alifika uwanja wa ndege huku akiwa anaandamwa na magari ya polisi.
“Uko chini ya ulinzi!” walisema askari polisi huku wakimfuata.
Alitoa kitambulisho chake akawaonesha kisha akasema; “Kuna kazi maalum nafanya hapa, nyie endeleeni kunipotezea muda, mambo yakiharibika mtajibu nyie,” alisema huku akielekea sehemu yenye madirisha ya ofisi za kampuni za kuuza tiketi za ndege.
“Unaweza kuniangalizia kama kuna ndege yoyote inayoweza kunipeleka Congo DRC siku ya leo?” Jabir alihoji kwa sauti ambayo ilimshtua yule mtoa huduma.
Hakujibu kitu, akaanza kupekua kompyuta yake, wakati akifanya hivyo Jabir akapata wasaa wa kusoma ule ujumbe wa simu uliokuwa umeingia wakati akiwa njiani kuja uwanja wa ndege. Ulisomeka “Utamkuta Goma, Central Faith Church, Runyoni. Una saa 24 tu!” Macho yakamtoka, akasikia midomo imemkauka halafu ulimi ukapotewa na mate kwa muda.
Wanaharamu hawa, mahayawani, nitawaonesha! Alijiwazia kwa hasira kali huku mikono ikitetemeka.
“Tukutane Goma!” Alifoka kwa sauti hadi watu wote eneo hilo wakageuka kumuangalia.
Yule dada mkatisha tiketi akabaki ametoa macho, halafu kwa sauti ya kutetemeka akasema.
“Hakuna tiketi siku ya leo kaka yangu….!”
“What…??! I need one. Fanya nipate tiketi!” Jabir alisema huku machozi yakimtoka.4

…M c h e z o H u u H a u t a k i H a s i r a


SAA kumi na mbili kamili jioni siku hiyo ya Ijumaa, ilikuwa na harakati nyingi.
Watu walijiandaa na mapumziko ya mwisho wa wiki, si kwamba siku zinabadilika inapokuja Ijumaa, ila ukweli ni kwamba mara nyingi watu hufanya vitu wanavyotakiwa kufanya ndani ya siku tano ila hufanya vitu wapendavyo kufanya kwenye siku mbili za mwisho wa wiki. Ndio maana huonekana kuwa siku maalum sana. Wengine walipenda kwenda nje ya jiji, wengine walipenda kwenda mapumziko na wapenzi wao halisi au wa kuazima.
Kwa wengine ilikuwa ni wakati wa Ligi ya Uingereza inayowaliwaza zaidi.
Lakini kwa watu walio kwenye mikakati yao kama hawa hapa, saa hii ilimaanisha kuwa saa kumi na mbili kati ya zile sabini na mbili zilizokuwa zimetolewa, zilikuwa zimeondoka. Ina maana kulikuwa na saa sitini tu zimebaki hadi kufikia siku ambayo Rais wa nchi hiyo na Tume ya Uchaguzi walitakiwa kutoa tangazo la tarehe ya uchaguzi. Hilo lingefanyika kwa amani ama kiroho safi kama tu huyu binadamu aitwaye Joesph Katanga angekuwa ameondolewa kwenye ramani ya walio hai. Kilichowaumiza vichwa wahusika kwenye operesheni hii ni kuwa kati ya hizo saa sitini, saa thelathini na sita zilikuwa ni usiku, ilimaanisha waongeze juhudi, maarifa na ufanisi ili waweze kwenda na kasi ya matukio na mambo.
Hatimaye mpelelezi Jabir Makame aligundua kuwa hasira hasara. Hasira ya mkizi siku zote humsaidia mvuvi, alijikumbusha, isingemsaidia chochote kama angekuwa katika hali kama ile. Alihitaji utulivu wa akili, utimamu wa mwili na hisia ili aweze kukabiliana na kilichoko mbele yake.
Baada ya kuambiwa kuwa hakukuwa na usafiri, alipiga hatua za kizembe hadi kwenye mabenchi ya kungojea kuingia ndani ya uwanja, alijiinamia kwa dakika kadhaa. Aliambiwa kuwa ndege nyingine ya kuelekea Kinshasa DRC ingeondoka saa kumi asubuhi siku iliyofuata.
Mara wazo likamjia kuwa huo ulikuwa ni muda mzuri wa kuendelea na upelelezi aliokuwa ameuanza asubuhi. Alifungua begi lake dogo akatoa lile faili ambalo alikuwa amepewa na Bi. Anita. Akalisoma tena na kujua mtu ambaye angeweza kujibu maswali yake baada ya Sadick Joseph.
Kwa nini walifanya biashara na kampuni kama ile? Huyo mtu aliyejitambulisha kwa Sadick kwa jina la ‘KK’ ni nani? Jabir alijiuliza huku akiwa anasimama. Aliona aingie kazini, hiyo ingekuwa njia bora ya kusubiri ndege ya saa kumi asubuhi. Haihitaji hasira!

* * *

Saa mbili na nusu usiku, gari alilokuwa akiendesha mpelelezi Jabir Makame lilipita kwa kasi mbele ya majengo ya ofisi za China Army Cargo. Mtaa ulikuwa mpweke sana wakati huu. Kulikuwa na mbwa kadhaa waliokuwa kwenye ‘burudani’ yao.
Mbwa wasio na nguvu za kushindania nafasi walijitia kubweka kwa hasira baada ya gari ya Jabir kupita. Walijifanya kukasirishwa na mwendo ule wa gari, kumbe ilikuwa ni sehemu ya kutolea hasira zao tu.
Alikusudia kupita kwa mwendo huo kusudi kuondoa uwezekano wa kutiliwa shaka na yeyote ambaye angeweza kuwa kwenye ofisi ile, hakuona mtu yeyote upande wa mbele wa ofisi hizo. Taa kubwa ilikuwa imewashwa na kufanya eneo lote la mbele lionekane vyema, aliendelea na kwenda kupaki mbele kabisa halafu akazunguka mtaa wa nyuma wa jengo lile. Huko alitembea haraka kuelekea upande ambao jengo lile lilikuwepo.
Begi lake lenye vitu vya safari aliliacha garini, baada ya kupenya hapa na pale, kuvunja hiki na kusogeza kile na kujikuta amechubuka kidogo, hatimaye alifanikiwa kuingia ndani ya ofisi za China Army Cargo kwa kupitia upande wa nyuma wa jengo hilo.
Jengo hilo lilikuwa na vyumba vitatu vya ofisi. Cha kwanza ni pale alipokuwa yule msichana wa mapokezi, cha pili kilikuwa kimeandikwa Country Representative, halafu upande mwingine kulikuwa na chumba kikubwa sana ambacho kilikuwa na meza saba zilizojitegemea ambazo zilionesha kuwa ofisi hiyo ilikuwa inakaliwa na wafanyakazi saba. Hakujisumbua na vyumba vingine, alianza kuhangaika na mlango uliokuwa umeandikwa ‘Country Representative’. Alijua fika kuwa chumba hicho ndicho alichokuwa anatumia Sadick Joseph ambaye sasa alikuwa marehemu.
“Tulia hivyohivyo!” alipewa onyo na sauti toka nyuma yake. “Dondosha chini bastola yako, ujanja wowote hutopata nafasi ya kuujutia kwa vile maiti huwa hazijuti!”
Jabir aliidondosha chini bastola yake.
“Piga hatua mbili toka kwenye huo mlango!”
Akatii. Baadaye akasikia hatua zinapigwa kuja pale alipokuwa amesimama, kisha akaanza kukaguliwa. Hakutaka kufa kikondoo, alitaka afe akiwa kwenye uwanja wa mapambano halisi.
Alimsukuma jamaa kwa nguvu wote wakaangukia chini, wakati huohuo akasikia bastola ikikohoa. Alijibiringisha hadi ilipokuwa bastola yake, kabla mkono haujaifikia ulipigwa teke, akajivuta na kuivuta miguu ya yule jamaa, akaanguka chini. Jabir akajua kuwa alikuwa anapambana na watu wawili. Alishamwona mwingine akiwa amesimama kwa mbali akihangaika namna ya kupata shabaha ili asije akamuua mwenzie.
Kwa kasi sana Jabir alichomoa kisu na kukirusha wakati akiwa anajibiringisha kwenda kumkumba yule aliyemvuta miguu. Kisu kikatua kwenye koo la yule aliyekuwa amesimama na silaha. Sasa hawa wawili wakawa wamesimama wanatazamana, Jabir akawa wa kwanza kujaribu bahati yake, akarusha ngumi na kuisindikiza kwa teke. Ngumi ikamkosa ila teke likampata, likampeleka chini, akamrukia na kumtia kabali.
“Wewe ni nani na umetumwa na nani?!” Jabir alihoji huku akipumua kwa fujo, akiwa amemdhibiti jamaa kwa kabali.
“Unajisumbua tu, hutojua chochote na hutofika kokote!” jamaa alisema kwa tabu. Jibu lake lilifanya Jabir aongeze kibano.
“Aaaaagggrrrri!!” jamaa alilalamika.
“Sema nani kakutuma?”
“Nimeekwaaambia, unajis….uuuu aaaaah!” jamaa akatulia ghafla.
Jabir akaweza kuhisi kulegea kwa yule jamaa hivyo akamwachia. Alikuwa ameshajiua kwa aina ileile ya kidonge cha sumu kama alivyokuwa amejiua Sadick, Jabir aliwakagua wale watu bila kuambulia chochote.
Alirejea tena kwenye ule mlango na kuanza kushughulika nao tena, zilimchukua kama dakika tatu hivi hadi alipofanikiwa kufungua mlango wa kile chumba.
“Tiiiiiiip,” mlio ulisikika mara alipoufungua mlango wa kile chumba. Hakujali sana, aliendelea na alichokuwa amekusudia kukipata. Alianza kupekua kila sehemu kwa ufundi mkubwa sana. Alifungua bahasha mbalimbali, mafaili, watoto wa meza na chochote ambacho alidhani anaweza kupata, chochote ambacho kinaweza kujibu moja ya maswali yake.
Akiendelea kuangalia akaona kasha jeusi limeandikwa kwa Kifaransa ‘Les acheteurs’ ikimaanisha Wanunuzi, akaliparamia haraka sana, kisha akaanza kutafuta alichokuwa akitaka kukiona, lakini kichwani akiwa amepata swali jingine; Kwa nini Sadick alikuwa anatumia Kifaransa kwenye maandishi yake mengi? Watanzania wengi hupenda kutumia Kiswahili au Kiingereza! Akiwa anaendelea kusoma mikataba ndani ya kasha hilo mara akaona alichokuwa anatafuta.
Meja Matungwa ndiye mtu Wangu, aliwaza. Haraka sana akachukua simu yake na kupiga.
“Phil, nitafutie mtu anaitwa Matungwa Ndebile, ni ofisa, Meja. Ndiye aliyesimamia mchakato mzima, cha ajabu ndiye aliyepokea vifaa vilivyonunuliwa, mtu mwenye cheo chake asingefanya hiyo kazi. Namba zake ninakutumia kwenye meseji, niambie yuko wapi saa hii!” Jabir alikata simu.
Papohapo akaandika namba ya Matungwa kwenye simu, hilo lilimridhisha sana Jabir ambaye sasa alikuwa ameanza kuchoka, chumba hakikuwa na hewa ya kutosha kwa vile hakuwa amewasha mashine ya kupoozea hewa halafu chumba hakikuwa na madirisha. Hivyo aliamua kutoka chumbani humo.
Akiwa mlangoni ndipo macho yake yalipoangukia kwenye kapu la kuwekea taka lililokuwa pembeni ya mlango kwa nyuma. Kulikuwa na karatasi tatu zilizokunjwakunjwa. Alizichukua na kuzikunjua. Alipofika ya pili alishangaa sana kuona tiketi ya ndege ya South African Airways, ikiwa na jina la Juliana Uwimana. Ndege hiyo ndio ileile ambayo Juliana mpenzi wake alikuwa amepanda mchana.
Mikono ikamtetemeka, hakutaka kuamini. Ina maana hawa ndio waliohusika na ukataji wa tiketi ya Juliana, inawezekana ndio walikuwa wanajiandaa kumteka. Lakini aliposoma vyema inaonesha kuwa tiketi hiyo ilikuwa kwenye mfumo wa baruapepe. Ilitumwa toka kampuni ya kuuza tiketi ya ndege kwenda kwa anuani ya baruapepe ya Juliana, halafu Juliana akaituma kwa Sadick na Kakengo Diamo akiweka ujumbe wa lugha ya Kifaransa pouvez-vous aider une femme enceinte à imprimer cela (Je, waweza kumsaidia mwanamke mjamzito ku print hii tiketi).
Hilo likamchosha kabisa Jabir, hakutaka kuamini, akajiona kama aliyechomwa mkuki moyoni. Inawezekana vipi? Juliana anajua kifaransa? Inawezekana kuwa hajatekwa? Jabir Makame akainyoosha vema ile karatasi na kuipiga picha kwa simu yake, halafu akaituma kwa Phil, ambaye ofisi fukuzi ilikuwa ikimfanya kama kompyuta, Jamaa alikuwa mtaalamu wa teknolojia ya mawasiliano na kwa vile alikuwa amepewa vifaa vya hali ya juu vya kijasusi, hakuna sehemu au kitu alikuwa anashindwa kupekua kwa kutumia teknolojia hiyo. “Can you check thi as well” (Je waweza niangalizia hii pia). Ndivyo alivyoandika Jabir baada ya kuwa ameituma ile picha ya tiketi. Alifungua mlango wa kile chumba kisha akaufunga nyuma yake, halafu ule mlio ukasikika tena, “Tiiiiiip!”
Hakujali. Akawa anapiga hatua kwenda kule alikokuwa ameingilia. Alipopiga hatua ya tano, mlipuko mkubwa sana ukatokea. Mlipuko uliotawanya kabisa lile jengo na moto mkubwa kufuata!

* * *

JOSEPH KATANGA alikuwa kwenye bwawa la kuogelea muda huu. Akifanya kitu alichopenda kukifanya, kitu alichojua kukifanya, alikuwa akiogelea kwa mbwembwe kwa namna ambayo usingeweza dhani kuwa mbele yako ulikuwa ukimuangalia mbabe wa kivita, mtu anayetafutwa na kuogopwa sana. Lakini maisha yake ya namna hii, maisha yasiyotabirika na kuwa sehemu ambazo vyombo vya kijasusi visingedhani kuwa angeweza kwenda, bila ulinzi na akafanya kitu cha starehe hadharani namna hii ndio ilifanya iwe ngumu yeye kuwekwa mikononi mwa adui zake.

Akiwa hana muda mrefu tangu atoke gerezani, akiwa anajitahidi kuanza kuzoea maisha ya uraiani huku yeye pia akiyapa nafasi maisha yaanze kumzoea, Joseph Katanga alikuwa ni yule yule. Yule yule ambaye kuonekana kwake ni kama Kakakuona. Alipoonekana mahali, vyombo vya usalama vilipokuwa vikipeana taarifa juu ya uwepo wake mahali fulani, hadi wanapokuwa tayari kwa ajili ya kumkabili wangekuta ameshatoweka. Ungeweza dhani kwa mtu kama yeye, kiongozi wa kikundi sugu cha waasi, angekuwa akiishi na kufanya kila kitu akiwa kwenye misitu ya Congo. Wengi walidhani hivyo lakini hayo hayakuwa maisha yake halisi, alipenda starehe, alijua kuzifanya kwa namna ambayo iliwakera adui zake na hata wakati mwingine walinzi wake.

Wazungu kadhaa na waafrika wachache waliokuwa sehemu hiyo ya kuogelea walijikuta wakiwa wanamhusudu mtu huyu aliyekuwa akiogelea kwa ufundi mkubwa, hivyo wakaketi nje ya maji wakiwa na wapenzi wao, glasi za mivinyo zikinyonywa taratibu, macho kodo wakimuangalia Katanga akiwa anafurahia maji. Pembeni upande wa Kaskazini wa bwawa hilo la kuogelea, ndipo alipokuwa ameweka nguo zake na vifaa vyake kadhaa. Huku msichana mmoja mbichi, mrembo akiwa amevaa bikini tu alikuwa akiviangalia. Pamoja na vitu vingine vichache vilivyokuwa hapo kulikuwa na vichwa vitatu vya simu za mkononi, simu hizo zilikuwa na rangi tatu tofauti; nyekundu, njano na kijani. Rangi hizo ziliwakilisha umuhimu wa mpigaji wa simu. Ya kijani ingekuwa ya kawaida tu, njano ya mtu wa wastani na nyekundu angeipokea hata angekuwa sehemu ambayo hakutaka kuongea. Nyekundu ilijulikana na watu muhimu sana, kijani watu wa kawaida sana, hasa wanaomjua kama mtu wa kawaida kwa maisha ya kawaida, njano ni watu ambao walikuwa katikati ya kijani na nyekundu.

Akiwa anaendelea kuogelea kwenye bwawa la hoteli hii ya kifahali iliyoko katikati ya kinshasa, mara yule msichana alipunga hewani ile simu nyekundu. Kwa jinsi aliyokuwa akiogelea, huku macho yakionekana kuwa yamefumbwa, usingedhani kuwa angeweza kuona wakati yule msichana akiipunga ile simu taratibu na kwa usiri mkubwa. Ghafla Katanga alikatisha safari yake ya kuogelea na kuanza kuelekea kule alipokuwa ameketi yule mrembo. Alipofika pembeni mwa bwawa jirani na alipokuwa yule msichana, aliisukuma juu miwani yake ya kuogelea hapo macho yake kama ya kinyonga yakaonekana. Alinyoosha mkono mmoja huku mmoja ukiwa umeshikilia chuma cha pembeni ya bwawa, mwili wote tokea kifuani kwenda chini ulikuwa ndani ya maji.
“Sema mpenzi!” Joseph Katanga alisema baada ya kuangalia namba ya mpigaji.
“Target namba 4 iko Hoteli Bambrass chumba namba 579” Sauti ya kike ilisema na simu ikakatwa. Simu ilipokatwa, mwili wa Joseph Katanga ulisisimka, alimeza funda kubwa la mate. Aliinua ile simu, yule mrembo akaipokea.
“Get ready, kuna windo pale Bambrass!” Katanga alimwambia yule mrembo kwa sauti ya chini, halafu kama anayejifanyia mwenyewe alinyanyua mkono wake juu akauzungusha na kufanya ishara fulani. Kwa watu waliokuwa wakimuangalia eneo hilo wangedhani alikuwa akijinyoosha tu, lakini vijana wake sita waliokuwa kwenye vyumba mbali mbali vya hoteli hiyo na hoteli za jirani, ambao walikuwa madirishani mwao wakiwa tayari na bunduki zao za kudungulia walimwelewa, hivyo wadunguaji watatu walianza kukunja bunduki zao maalum za kundungulia tayari kwa kuondoka, huku watatu wakiendelea kumuangalia kwa kupitia darubini zilizokuwa sehemu ya hizo bunduki zao za kundungulia.
Huu ni utaratibu wa kawaida ambao Joseph Katanga amejiwekea, huwa kuna wadunguaji, yaani, ‘Snipers’ wasiopungua sita ambao huwa popote anapokuwa. Huwezi kuwaona lakini ni watu ambao huwa umbali wa mita kadhaa toka anapokuwa. Huwa wamejificha, bunduki zao tayari kwa shambulizi lolote, kazi yao kubwa ikiwa ni kuangalia anapokuwa Katanga na maeneo ya jirani. Hii hufanya maadui wake ambao wamebahatika kubaki wao na yeye kufa kwa namna ambayo huwaachia maswali mengi sana wale waliowatuma. Wengi hudhani kuwa anatumia ndumba kujilinda na kukabiliana na adui zake.
Alitoka majini na kuvaa. Dakika Ishirini baadaye alikuwa anaingia Hoteli Bambrass kama alivyokuwa amedokezwa na mpasha habari wake. Kama kawaida hakuwa ameambatana na mtu mwingine yeyote zaidi ya yule msichana aliyekuwa naye bwawani. Safari hii alikuwa amevaa gauni refu kama kanzu hivi, miwani mizuri ya thamani kubwa, huku yule msichana mrembo akiwa amevaa kama binti wa kiarabu mshika dini, waliingia Bambrass Hoteli na kwenda moja kwa moja kwenye chumba walichokuwa wameelekezwa. Walipokuwa wakipita mapokezi waliona askari wanne wa jeshi wakiwa hapo, hii ilimthibitishia kuwa mtu aliyekuwa ameambiwa kweli alikuwepo. Maana mtu aliyekuwa anamwendea alikuwa mtu mwenye cheo cha juu sana kwenye jeshi la Congo ambaye alikuwa na kisasi naye hasa kwa kuchangia kwa kiasi kikubwa kwenye kukamatwa kwake na kupelekwa ICC.
Walipofika kwenye mlango wa chumba 579, Katanga alifanya ishara yule msichana alisogea pembeni. Mlango wa chumba ukagongwa halafu yule msichana akasema kwa kifaransa “Service de chambre, s’il vous plait” ikimaanisha “Huduma ya chumba tafadhali”. Halafu wakasubiri kwa muda kidogo kabla ya mlango wa chumba kufunguliwa kidogo tu na sauti nzito kusikika “Je n’ai pas besoin” ikimaanisha “Sihitaji”. Lakini kabla aliyesema hajarudishia mlango, mlango ukasukumwa kwa nguvu na Joseph Katanga. Katanga akawa ameshajaa ndani na kukutana na watu wawili waliokuwa uchi wa mnyama, Jamaa alipomuangalia tu Katanga usoni akamtambua. Mara akabadilika kuwa mbogo, akiwa uchi akarusha ngumi moja nzito iliyotua shingoni kwa Katanga. Katanga akapepesuka na kujiweka sawa.
“Bitch!!” Jamaa akatukana, Katanga akatabasamu, Jamaa akarusha teke moja zuri, Katanga akaliona na kuudaka mguu, kwa nguvu ambazo usingedhani kuwa Katanga kwa mwili wake ule angeweza kuwa nazo aliufyatua ule mguu kwa kasi sana. Jamaa akapiga kelele lakini hakupata kumaliza akapigwa teke safi la shingoni, wakati huo wale wasichana wawili walikuwa wakiwaangalia tu mafahali wakioneshana kazi. Jamaa akaenda chini, wakati anataka kuinuka, uti wa mgongo wake ulipokea pigo zito toka kwa Katanga ukavunjika. Jamaa akawa hoi amelala chini. Jamaa alitoa macho mabaya ya kutisha.
“Mwache huyu msichana aende zake, hana kosa lolote!” Jamaa alisema kwa sauti yenye maumivu makali huku akipumua kwa fujo.
“Ha ha ha ha, unajua vema kanuni zangu, au wadhani gereza limeweza kuzibadili kama wanavyodai” Joseph Katanga alisema halafu akatoa bastola na kumpiga yule msichana wa yule mwanajeshi kwa risasi moja tu ya paji la uso halafu akamgeukia yule mwanajeshi.
“Naitaka nchi yangu, naitaka Congo.” Halafu akamtandika risasi tatu za kichwani. Wakati huo huo wakasikia vishindo vya watu wakija kwenye chumba walichokuwa. “Twende zetu mrembo!” Alisema halafu wote wakaelekea kwenye dirisha la chumba hicho ambacho kilikuwa orofa ya tano, kwa namna ya ajabu sana walitumia dirisha hilo kushuka hadi chini ya jengo hilo.
__________________

Saa tatu kasorobo usiku, ndani ya Jiji la Dar es Salaam.

“Ndege hii ni ya chama cha madaktari wasio na mipaka, itaondoka baada ya saa moja kuanzia sasa. Kwenye huu mkoba tumeshakuwekea nyaraka zote ambazo utazihitaji kwa ajili ya safari hii. Ukifika Kinshasa utakuta teksi namba KF91X ikiwa inakungoja, hiyo itakupeleka sehemu ambayo utakuta vifaa vyako vyote vya kazi,” Bi. Anita alisema huku akiwa anamuangalia Jacob Matata kwa macho ya udadisi.
“Kifo cha Jabir Makame, utata wa ukweli kuhusu mke wake, usaliti dhidi ya wale makomandoo vinanifanya nisimuamini yeyote,” Jacob Matata alisema huku akijiweka vizuri kitini. “Je, kwenda kwangu Congo DRC kunajulikana na watu wangapi? Nataka niwajue majina yao wote ili nikae nikijua!”
“Kwa hapa ofisini hakuna ajuaye zaidi yangu” Bi. Anita alisema. “Uamuzi huu nimeufanya baada tu ya kusikia taarifa za kifo cha Jabir Makame. Labda mtu wetu anayeshughulikia kuchapisha nyaraka bandia ndiye anaweza kuhisi kuwa unasafiri, kwa vile ile pasi ya kusafiria ilibidi aweke jina lako. Lakini mimi mwenyewe nimeiingiza kwenye mfumo wa Uhamiaji ili itambulike na mashine za pasi za kusafiria ukiwa sehemu za ukaguzi, hivyo nitasema ni mimi na yeye kwa hapa Tanzania, labda na dereva utakayemtumia ukiwa unakwenda uwanja wa ndege baada ya kikao hiki,” Bi. Anita, alieleza.
“Na huko Congo, umesema dereva wa teksi ambaye atanipeleka kwa huyo mtu….!” Jacob alisema halafu kauli yake ikakatishwa na Bi. Anita.
“Bwana Mbanga Mbia Mbanga alikuwa mkuu wa upelelezi wa DRC ambaye alistaafu mara tu baada ya utawala wa Kabila mkubwa kuangushwa, kwa hivyo kwa sasa yupo tu, najua dereva atakayemtuma wala hatojua wewe ni nani, kwa heshima iliyopo baina yetu amekubali kukupokea na kukupa taarifa nyingine za muhimu zaidi ya hizi nilizokupa!”
“Okay, kwa hivyo kazi ni mbili tu; Joseph Katanga na ukweli kuhusu Juliana Owima ambaye dakika za mwisho imekuja kujulikana kuwa ni Juliana Uwimana. Na natakiwa niende pale walipotaka Jabir Makame aende, yaani, Central Faith Church, Runyoni mjini Goma. Unafikiria nini kuhusu operesheni hii?” Jacob Matata aliuliza.
Kwa kifupi Jacob ameshafanya kazi na huyu mama kwa muda mrefu, wamepitia mambo mengi magumu pamoja. Jambo moja ambalo ana hakika nalo ni kuwa mama huyu huwa anafikiri kwa kasi na ufasaha sana, anajua sana kutabiri mienendo ya matukio. Hivyo hupenda kuuliza ushauri wake wakati anapokuwa anakabiliwa na kazi ngumu kama hii.
“Well, nadhani uko kwenye nafasi nzuri, hawa watu kuna mambo mawili; kama hawajapata taarifa za kifo cha Jabir Makame basi watakuwa wanamtarajia uwanja wa ndege kesho asubuhi, kwa vile tayari wanajua kuwa ndege inayofuata toka Tanzania itatua Kinshasa asubuhi. Ndio maana nimetaka wewe uende usiku huu ili uonane na mzee Mbanga Mbia Mbanga, ili asubuhi wakati wanamsubiri Jabir Makame na wewe uwe hapo ili ikiwezekana uwaone waliokuwa wakitarajia ujio wa Jabir Makame.”
“Unaweza kuanzia hapo, lakini hata kama wana taarifa za kifo cha Jabir Makame, bado watataka kujiridhisha maana mtu anayesemwa kufia kwenye jengo na mwili wake usipatikane huwezi kuwa na uhakika kama mtu alifia humo, kwa hivyo kama ni watu makini, najua wako makini kwa waliyofanya hadi sasa lazima bado watatuma mtu ili kuhakiki” Bi. Anita alisema huku akiminya midomo yake ya chini kwa vidole vyake.
“Mmmmh napata mkondo wa mawazo yako, nitafanyia kazi. Vipi kuhusu makomandoo wetu wawili, unadhani mambo yakoje?” Jacob alizidi kudodosa.
“Nadhani ni ngumu sana kupata picha halisi maana jambo lao limegubikwa na utata mkubwa,” Bi. Anita alisema huku akiwa anasimama. “Ila najua Goma kutakuwa na mpambano wa kufa na kupona, lakini kama ungeweza kumpata Twaha Mchoppa ili muunganishe nguvu kwenda kumuokoa Pablo Mahene na kumuondoa Joseph Katanga hiyo itakuwa muvi nzuri sana. Ila ukweli Goma ni kazi kwelikweli, najua haitokuwa kazi rahisi kumuua mtu aliyekubuhu kama Joseph Katanga.”
“Una dakika hamsini kuwa uwanja wa ndege,” aliongeza. “Hivyo nadhani ni wakati mwafaka wa kuondoka. Nakutakia kila la kheri Jacob Matata, nimechukua uamuzi huu kutokana na uzito na hali iliyojitokeza katika suala hili, tuna saa chache sana za kutekeleza misheni hii, hivyo nimeona dawa ya moto ni moto. Kwa vile wao wanafanya mambo yao kwa namna hii acha sasa tuone itakuwaje.”
“Dawa ya moto ni moto ila tuombe Mungu, sasa kutokana na huu muda itabidi nichukue pikipiki hadi nyumbani kwangu, maana kwa hii foleni ya Dar muda huu naweza chelewa ndege, ndege yenyewe ya msaada” Jacob Matata alisema huku akiwa anasimama tayari kuondoka.

* * *

Nusu saa baada ya mazungumzo ya Bi. Anita na Jacob Matata, Joseph Katanga alikuwa amesharejea kwenye moja ya vyumba vyake vya siri baada ya kufanya alichokuwa ameenda kufanya Hoteli Bamprass, Kinshasa Congo DRC.

Mlango wa chumba alichokuwa uligongwa. Yule msichana mrembo aliingia akiwa amebeba simu nyekundu. Aliichukua na kuiweka sikioni.
“Sema mpenzi!”
“Jacob Matata kapewa kazi!” Sauti ya kike iliongea simuni.
“Tumia watu wetu walewale walioko Tanzania waende nyumbani kwake sasa hivi wakammalize, lakini wape taarifa wale watu niliosema wachunge uwanja wa ndege” Katanga aliongea kwa sauti ile ile ya taratibu utadhani anatongoza mwanamke anayemhusudu sana.
“Waambie huyo mtu ni hatari sana, hivyo wachukue tahadhari zote na watumie hata fursa finyu sana wapatayo kuhakikisha haondoki Tanzania” Katanga aliongeza.
“Sawa halafu target namba 2 yuko kijijini Kiota, nasikia ana kikao cha siri pale!” Ilisema ile sauti ya kike.
“Asante, naona leo uko kwenye kiwango cha juu cha ufanyaji kazi!!” Katanga alisema kwa furaha na kukata simu.
“Tunakwenda Bunagana a.k.a Paradiso ya Jose Katanga, kuna kazi ya kufanya pale kijijini Kiota!” Katanga alimwambia yule mrembo halafu akageukia ukutani, yule mrembo akainama kwa heshima halafu akaondoka. Katanga alikwenda kwenye sinia lililokuwa na matunda na kuchukua vipande kadhaa vya matunda na kutupia kinywani. Alitafuna huku amefumba macho! Safari hii alikuwa kwenye moja ya vyumba vya vyake vya siri vilivyo kwenye mitaa ya kawaida kabisa iliyopo Kinshasa.


Ilipofika saa tano usiku baadaye tayari alikuwa ameshawasili Goma, kwenye ile kambi yake tukufu iitwayo Paradiso.
Ndani ya jengo liitwalo The Rock, Joseph Katanga alikuwa ameketi kwenye mkeka kwa ule mkao wa wacheza Yoga, pembeni yake kukiwa na kisu na sinia lililojaa matunda. Zaidi ya mkeka aliokuwa amekalia, kisu na lile sinia la matunda hakukuwa na kitu kingine mle chumbani. Labda cha ziada ni ile ramani kubwa ya nchi ya Congo DRC iliyokuwa ukutani. Alikuwa amevaa kaptula nyeusi na tisheti ya kijani, alioneka kuwa mtulivu, mara kwa mara alichukua kipande cha tunda toka kwenye sinia na kukibugia chote mdomoni halafu alipoanza kutafuna alifumba macho kusikilizia utamu.

Baada ya muda alisimama, akaenda kusimama dirishani, dirisha ambalo lilikuwa likitazamana na pori lililokuwa upande wa Magharibi mwa kambi hiyo. Alisimama hapo kwa muda hadi pale mlango wa chumbani kwake ulipogongwa, aligeuza kichwa taratibu na kuuangalia mlango uliongogwa. Ulipogongwa kwa namna fulani ndipo Jose Katanga aliposema “Bunagana a.k.a Paradiso ya Jose Katanga”. Halafu sauti ikasikika ikisema “Amani”. Aliposikia jibu hilo akaenda mlangoni na kuufungua mlango ambao hata hivyo ulikuwa umerudishiwa tu. Kwa hivyo kugonga lilikuwa swala la heshima tu na kuzingatia kanuni lakini halikuwa suala la usalama. Aliingia kijana mmoja aliyekuwa na sura ya kutisha, hata baada ya kuingia ndani kuna halufu ilisikika.
Katanga alimuangalia yule kijana kwa muda halafu kwa sauti tulivu kabisa akasema; “Leta habari Pichou”
Yule kijana aliposikia hivyo akainama kama heshima.
“Tanzania mambo yamekwisha, mpelelezi waliyemuweka ameshauawa na vijana wetu sasa......” Kauli ya yule kijana ilikatishwa na kicheko cha Joseph Katanga, meno yake meupe na yaliyopangika vema yalionekana na kufanya uzuri wake wa kiume uonekane.
“Nani kasema yamekwisha? Wewe sema Makame ameuawa lakini usiseme yamekwisha, nadhani huwajui watanzania wewe! Weka watu uwanja wa ndege kuanzia sasa hadi keshokutwa, hakikisha kila mtu anayeingia mwenye dalili zisizofaa anachunguzwa vema. Sitaki makosa, naitaka Congo yangu!” Joseph Karanga alisema halafu akageukia ule ukuta wenye ramani. Yule kijana alipoona hivyo aliinama tena kwa heshima na kutoka mle chumbani. Hakuchukua muda naye akatoka, akaenda kwenye chumba kingine ambamo hakuchukua muda akatoka akiwa amevaa magwanda ya jeshi. Alitembea hadi sehemu iliyokuwa inaonekana kama chumba cha maongezi. Hapo aliwakuta watu wanne wakiwa wamesimama, alipofika wale askari walimpigia saluti halafu naye alapiga saluti.
“Tunaendelea na kazi zetu, nasikia meja Moisa yupo hapo kijiji cha jirani kwa shughuli ya siri, nataka niende nanyi sasa hivi ili tukamuue. Kama kawaida mara zote kabla sijaenda kwenye kazi kama hii huwa napenda kukumbusha mambo matatu. Mnayakumbuka?” Katanga alisema huku akiweka vema silaha zake. Halafu wale askari wanne wakaongea kwa sauti za pamoja;
Ua upendavyo!
Usisite kuua!
Furahia kuua!
Msamaha hutolewa na Katanga tu!
Walisema kijeshi kwa sauti za kujipandisha midadi.
“Vema, haya twendeni!”

* * *
Saa saba na nusu usiku Katanga alikuwa amesharejea kwenye himaya yake, kazi yake ya kuimaliza tageti namba 2 ilikuwa imeshakamilika. Ni wakati huo hakukaa sana chumbani, alivaa kanzu na kutoka nje. Alitembea taratibu kuelekea vichakani, hakuwa na mlinzi yeyote. Safari yake hiyo ya kushitukiza, ambayo hata walinzi wake hawakuwa na taarifa nayo ilimfikisha kijiji cha jirani, kijiji kilichopewa jina la utani ‘Kiota Village’. Kwa jinsi kijiji hicho kilivyokuwa tulivu japo kilikuwa katikati ya uwanja wa vita ya waasi na serikali. Wanakijiji wa kijiji cha Kiota walikuwa wameshaingia kwenye nyumba zao za nyasi. Kijiji hicho ambacho kina mahusiano mazuri na waasi hao wanaoongozwa na Joseph Katanga, walishaamuliwa kuwa wanaingia vitandani mwao mapema kwa sababu za kiusalama.
Katanga alitembea kwa kunyata hadi alipofika kwenye nyumba aliyokuwa amekusudia. Ilikuwa nyumba ya nyasi kama nyingine nyingi eneo hilo, badala ya kwenda mlangoni alikwenda dirisha la upande wa kushoto, lilikuwa dirisha lililofanywa kwa madebe yaliyokatwa katwa. Alipofika dirishani alisimama kwa dakika kadhaa akiwa kimya kabisa.
“Kho kho kho mmmmh!” Kikohozi hafifu kilisikika toka ndani. Katanga akapiga mluzi mmoja hafifu halafu alitulia.
“Khoo Khoo Khoo mmmmh!” Kikohozi kilisikika tena. Halafu kama mwanzo, Katanga akapiga tena ule mluzi hadifu.
“Nani?” Sauti ya kiume ambayo ilisikika wazi kuwa ilitoka kwenye koo lililochoka kwa kutumiwa miaka mingi ilisikika.
“Rais” Katanga alinong’ona halafu akatulia. Sekunde chache baadaye mlango wa bati ulisikika ukifunguliwa. Katanga akaingia.
“Oooh mwanangu, nimefurahi umekuja, nilisikia taarifa kuwa umerudi, nilishaanza kukata tamaa kuwa ningekufa bila kukuona tena!” Alisema yule mzee wa kikongo huku akimkumbatia Katanga. Kibatari kikawashwa na maongezi yakaanza. Waliongea kama watu wanaojuana sana kwa undani. Sasa katanga akawa anaongea kama mtu anayeongea na mzazi wake.
“Sikupoteza matumaini, rafiki zangu walikuwa wakija kunitembelea gerezani na kuniarifu kila kilichokuwa kikiendelea. Nashukuru walifanikiwa kuendelea kulinda eneo hili na ninyi, kweli KK ni mwanaume. Itakuwa shangwe sana siku ambayo tutatandikiwa zuria jekundu na kuingia Kinshasa na kuichukua nchi yetu toka mikononi mwa hawa wakoloni weusi” Katanga aliongea kwa sauti ile ile ya utulivu sana.
“Hujabadilika mwanaume, uko vile vile, nimesikia ambavyo asubuhi hii umeichukua roho ya meja Moise, wanakijiji wote ndio wamehakikisha kuwa umerejea. Inasemekana wauaji walikuwa wastarabu, walioua kwa kusherehekea na hawajasamehe mtu. Niliposikia nikajua jembe langu limerudi” mzee alisema kwa furaha utadhani walikuwa wakiongea mambo ya kufurahia.
“Aaaah Mzee Kasheba, nilikuwa nina kiu sana na shughuli kama hizi, napenda hii kazi....!”
“Sasa siku ukiwa Rais utafanyaje maana hutokuwa unafanya hivi?” Yule mzee alimkatisha katanga.
“Kila jambo na wakati wake!” Katanga alijibu kifupi.
“Ila jasiri haachi asili!” Alisema yule mzee.
“Vipi kuna habari yoyote muhimu kwangu hapa kijijini?” Katanga alihoji.
“Hapana la muhimu zaidi ya simulizi ya namna umemuua Moise na timu yake!” Mzee yule alijibu. Baadaye mazungumzo yaliendelea kwa muda mrefu. Walipokuwa wameridhika, Joseph Katanga aliondoka nyumbani kwa mzee Kasheba na baadaye akaondoka kijijini hapo kama mzimu kurejea kwenye himaya yake.

_________________


MPELELEZI Jacob Matata aliwasili nyumbani kwake akiwa juu juu anafukuzana na muda. Baada ya kuegesha chini ya mti ile pikipiki aliyokuwa ameitumia, Jacob Matata, kijana mwenye umri kati ya miaka 38, mrefu, mwenye mwili wa wastani, ambao usingeweza dhani ni Komandoo aliyekamilika hadi pale ambapo ungemsogelea kwa karibu ili uone jinsi mwili huo wa wastani ulivyokuwa umefungana vema kwa mazoezi yenye kufuata ratiba kamili, uso wenye mvuto hasa kwa viumbe wa jinsia ya kike, nyele fupi zilizotunzwa vema. Alikuwa amevaa suruali aina ya jeans nyeusi na shati la mikono mifupi la rangi ya bluu. Alipiga hatua ndefu za kikakamavu toka pale alipoegesha pikipiki kuelekea ulipokuwa mlango wa kuingilia ndani ya nyumba. Alipitiliza moja kwa moja chumbani kwake na kuanza kuchukua vitu ambavyo angevihitaji kwa ajili ya safari yake hii nzito ya kushitukiza, alijua alikuwa anahitaji nini, hivyo hakuchukua muda mrefu.
Alitoka akiwa na begi dogo la kamera na vifaa vichache.
Ni wakati ameshamaliza mchakato huo akiwa amesimama sebuleni akiwa na mizigo yake ndipo alipohisi kuwa kulikuwa na kitu cha tofauti. Wakati anataka kuchukua silaha yake akawa amechelewa nukta chache.
“Tulia hivyohivyo bwana Jacob Matata” alisema yule mtu huku akimsogelea.
“Tumetumwa kwa kazi moja tu ya kukuua, ila nataka kukua kwa mkono wangu mwenyewe badala ya risasi” Kusikia hivyo Jacob Matata akatabasamu.
“Dondosha kila kitu!” Akapewa amri nyingine. Akadondosha mizigo aliyokuwa amebeba halafu akaangalia saa yake.
“Futa kabisa mawazo ya safari, maana hakuna maiti ambayo husafiri yenyewe, maiti huwa inasafirishwa, sasa hakuna ambaye atasafirisha maiti yako!” Jamaa alisema kwa kebehi huku akijiweka sawa kwa mapigano.
Kwa kasi ambayo yule jamaa na wenzie watatu hawakutarajia Jacob Matata alitoa na kurusha kisu na wakati huohuo yeye mwenyewe akajirusha. Kisu alichorusha kilitua kwenye koo la yule jamaa aliyekuwa na maneno mengi. Wale jamaa wenzie watatu risasi zao zilizokuwa zimeelekezwa alipokuwa amesimama Jacob Matata zilikutana na hewa. Wakati anatua chini Jacob Matata alichomoa bastola yake kwa kasi ambayo haikuwa rahisi kwa wale jamaa kuimudu. Risasi moja ikamwingia jamaa mfupi aliyejazia kama zile sanamu za Michelin, kuona hivyo jamaa mmoja akakimbia nje.
Kitendo kilichomshangaza mwenzie na kujikuta anapoteza umakini, Jacob Matata naye alikuwa akifukuzana na muda kichwani mwake aliliona kabisa tendo la yule jamaa aliyemshangaa mwenzie, risasi moja safi ikatua kwenye paji lake la uso na ikamsukuma chini. Halafu Jacob Matata akakimbia nje kumuwahi yule jamaa aliyetoka. Alikuwa ndio anamalizia kuupanda ukuta wa uzio ili adondokee upande wa nje. Risasi ya Jacob Matata kwenye bega la kulia ikamvutia ndani, akaanguka kama mzigo, Jacob akaanza kukimbilia alipoangukia yule jamaa. Wakati amemkaribia akamwongezea risasi nyingine ya mguu.
“Aaaaah fala sana wewe!” Jamaa akatukana na kumalizia kwa tusi la zito la nguoni huku akiugulia maumivu, Jacob Matata akamtamdika teke la mdomoni halafu akainama na kumbana mdomo kwa ile staili watumiayo wamama kumlazimisha mtoto kunywa uji. Akamnyang’anya silaha yake, halafu haraka haraka akachomeka kidole mdomoni mwa yule jamaa, akapekenyua chini ya ulimi na kutoa kile kidonge cha sumu.
“Haya sasa usinipotezee muda nataka uniambie nani amewatuma kuja kwangu na kwa nini?” Jacob alisema huku alikanyaga kwa nguvu lile bega alilokuwa amelipiga risasi.
“Aaaaaah, mwana wa malaya wewe hebu niue tu kuliko kunifanya hivi!” Jamaa alitoa kilio cha uchungu wakati Jacob Matata alipokanyaga jeraha lake kwa nguvu. Akakanyaga kama mara tatu hivi kitendo kilichomfanya jamaa awe hoi.
“Haya jibu swali langu” Jacob alisisitiza.
“Mimi sijui, yule mkubwa wetu ndiye alikuwa anajua”
“Mkubwa wenu ni yupi?”
“Yule aliyekuwa anataka kupigana na wewe!”
“Aliwaambia nani alikuwa akimpa amri?” Swali hilo la Jacob Matata lilimfanya yule jamaa kusita kusema, Jacob akakisukasuka tena kile kidonda kwa teke kali.
“Aaaaaaah sijui, ila huwa nilikuwa nikisikia akimtaja KK, sijui zaidi ya hivyo!” Jamaa aliongea kwa kilio.
“Huyo KK yuko hapa Tanzania?” Jacob alipouliza alikisuka tena kile kidonda kwa fujo.
“Aaaaaah mshenzi wewe, hustahili kuishi mwana wa shetani wewe!” Jamaa alilaani kwa jazba, lakini jeraha lake ambalo sasa lilikuwa likionekana kwa namna ya kutisha liliposukwa tena akaropoka.
“Hapanaaaaa hapanaaaa haap, namba haikuwa ya tanzania japo sikujua ilikuwa ya nchi gani, nasema kweli aisee niache nakuomba!!” Jamaa alipiga kelele.
“We si unajifanya mwanaume sasa mbona walia kama mwanamke? Swali la mwisho, ni muda gani ambapo mlipewa amri ya kuniua?” Jacob alipouliza alinyanyua mguu ili kukanyaga tena jeraha. Lakini safari hii akawahi kusema.
“Stop, stoop nasema, naeleza!! Nusu saa iliyopita!” Jamaa alipojibu tu Jacob Matata alimpiga risasi ya kichwa na kuelekea ndani.
Dakika chache baadaye alikuwa tayari akiwasha pikipiki ila akaona ni vema ampigie simu Bi. Anita kumuambia yaliyotokea.
“Wameshajua kuwa nimepewa hii kazi na nimeshaua wanne hapa nyumbani kwangu, hii ina maana tuna tatizo kubwa ndani, nadhani inafaa kufanya upekuzi mkubwa wa ndani, hii ina maana hakuna siri tena na nitakuta nasubiriwa Kinshasa, Sasa inabidi niwe makini sana na nitumie mbinu mbadala!” Jacob Matata alisema.5


L a z i m a K w e n d a G o m aGoma DRC – Kambi ya Jeshi

BAADA ya kugundua kuwa wenzie wote walikuwa wamekufa, ndipo akajua kuwa yale matone ya maji toka bombani halikuwa suala la bahati mbaya. Hakuona ni busara kujua nani alifanya ule mpango japo ingekuwa rahisi tu, lakini katika mazingira kama yale hilo halikuwa suala la kumshughulisha.
Sikutumwa kuja kufanya upelelezi bali kumuondoa Joseph Katanga, alijikumbusha kimoyo moyo. Kuombolezea wenzake isingemsaidia. Hilo angelifanya akirudi salama.
Kukimbia misheni ingekuwa kama kuwatukana wenzake, kukimbia kazi ambayo wamekufa wakiwa katika jitihada za kuikamilisha. Hiyo haikuwa sawa na alivyofunzwa. Alifunzwa kuwa njia bora ya kuwaenzi waliokufa wakiwa kwenye uwanja wa mapambano ni ama kushinda vita au na wewe kufia vitani, kamwe usigeuze mgongo kwenye vita iliyochukua maisha ya wapiganaji wenzio.
Hizo ndizo kanuni za komandoo.
Kufa kwa ajili ya nchi ni utukufu.
Risasi moja ikitumiwa vema, ikaingia kwenye kichwa kimoja tu cha mtu mmoja tu inaweza kubadilisha mwelekeo wa Congo DRC kuliko mapigano ya majeshi ya miaka 100. Aliwaza kwa sauti. “Lazima niingize risasi kichwani kwa yule kichaa Katanga”. Twaha Mchoppa alijiapiza kwa uchungu huku macho yake yakiwa mekundu kwa uchungu, hakutegemea mchezo ungebadilika kwa kasi namna hii. Kuwapoteza wenzie wote ndani ya masaa machache namna ile wakati hata kazi yenyewe haijaanza, hii ilikuwa imehitimisha zile hisia zake zilizomuambia kuwa kazi hii ilikuwa moja ya kazi za hatari kubwa.
Wakati king’ora cha kuwahadhari wapiganaji waliokuwa kwenye kambi ile kikilia na kuwakusanya uwanja wa kukusanyikia, yeye alipenya kwenye vichaka kadhaa na kuelekea sehemu ambayo waliambiwa kuwa wangekuta gari waliokuwa wameiomba kwa ajili ya kazi yao. Akili ilishamwambia kuwa yeyote aliyehusika au waliohusika kuwaua wenzie angekuwa hapo kuona kama kuna makosa yalifanyika ili amalizie kazi hiyo. Hivyo haikutakiwa ijulikane kuwa yupo, bora waanze kumtafuta kuliko kujipeleka kwenye macho ya muuaji.
Naam, alipofika eneo ambalo alitegemea kukuta gari walilokuwa wameomba, aliliona Spartan 4 X 4 likiwa limeegeshwa. Kabla ya kuingia kwenye lile gari aligeuka na kuangalia jengo alilokuwa ametoka, ilimuuma sana kujua kuwa miili ya makamanda wenzie ilikuwa imelala ndani ya majengo yale ikiwa haina uhai.
Mambo yalikuwa yametokea kwa haraka sana.
Twaha Mchoppa alifanya ishara ya kusali halafu akaparamia lile gari. Hakusubiri ruhusa, aliingia na kufunua tandiko la chini, akauona ufunguo. Akalitia gari moto na kuliondoa kwa kasi. Badala ya kuelekea upande ambao kulikuwa na barabara ya kuelekea kwenye msitu ambao kulikuwa na eneo linalotisha liitwalo Bunagana a.k.a Paradiso ya Jose Katanga, yeye alielekea Goma mjini kwanza. Ilikuwa saa sita na nusu za mchana.
Aliendesha gari kwa nusu saa, bila kuwa na dalili za kufuatwa na yeyote. Mwanzo alihisi huenda Meja Kabananga angemzuia asiondoke, hivyo alitarajia magari yangemfuata kumzuia, lakini inaonesha kuwa Meja Kabananga aliamua kumwacha aendelee na mipango yake. Hilo lilimfurahisha sana Mchoppa.

Ni jambo la kawaida kwa mji wa Goma kuonekana gari la jeshi kama lile likiwa linazunguka mitaani. Alipofika sehemu fulani alisimamisha gari, halafu akavua kiatu chake cha mguu wa kushoto, akakigeuza nyuma kwenye kanyagio, hapo akawa makini kuangalia maandishi yaliyokuwa yameandikwa kwa wino mzito wa rangi ya njano. Alipojiridhisha kuwa ameelewa kilichoandikwa alikivaa tena kile kiatu.

Akaliingiza gari barabarani na kuelekea mtaa wa wajasiliamali. Mji mchafu, ambao usingechelewa kujua kuwa umenajisiwa sana na vita nyingi ambazo zilifanya hapo kuwa makazi yake. Sehemu kubwa ya watu wa Goma hutumia kiswahili kama lugha ya mawasiliano. Hivyo mitaa yake mingi imepewa majina ya kiswahili, wenyewe wanasema kiswahili ni lugha yao ya taifa. Magari mengi ya majeshi ya jeshi la umoja wa mataifa, mashirika ya misaada ya kimataifa, majeshi ya serikali yalionekana yakiwa yametapakaa mitaani, kwenye barabara mbaya mbovu na chache zilizofanya mji wa Goma. Hadi alipofika kwenye ule mzunguko maarufu sana mjini Goma, yaani, ‘roundabout’, mzunguko wenye sanamu ya mtu akiwa anaendesha baiskeli, wenyewe wanauita ‘Chikudu Tshukudu’. Komandoo Mchoppa aliiangalia ile sanamu wakati akiwa anauzunguka huo mzunguko. Alipoumaliza akaingia kulia kwake na sasa akawa kama anatoka nje ya mji. Aliendesha lile gari kwa mwendo wa wastani hadi alipotoka nje kidogo ya mji. Sasa akawa ameingia kwenye mitaa ya vigogo kwenye eneo maarufu lijulikanalo kama Kanyamuhanga, sehemu inayodhaniwa kuwa na usalama kiasi kulinganisha na maeneo mengine ya Goma ambayo yako hovyo kiusalama. Eneo hili la Kanyamuhanga ndilo ambalo kuna mahoteli ya maana na ofisi za huduma kubwa kubwa muhimu kama mabenki na mawasiliano. Alipofika eneo hilo akaendesha hadi alipoona kibao kilichoandikwa Boulevard Kanyamuhanga et Avenue Butembo. Hapo akaanza kuangalia nyumba kubwa kubwa za kifahari zilizokuwa kwenye mtaa huu wa Butembo. Mtaa ulikuwa kimya kabisa huku nyumba nyingi zikionekana kuwa na vifaa vya kisasa vya usalama, aliendesha taratibu hadi pale macho yake yalipoona kibao cha nyumba P-1 Butembo 309, aliiangalia kwa makini sana wakati akiipita nyumba hiyo, aliweza kukiona kibao kilichochoka cha kampuni ya ulinzi kilichoandikwa ‘Eagle Eye Security Company’. Halafu katikati ya lango kuu la kuingilia kwenye ua wa nyumba hiyo kulikuwa na plastik imebandikwa yenye maneno HOUSE FOR RENT – CALL 0980x980. Twaha Mchoppa alimeza mate, akaiendesha Spartan 4 x 4 kwa mwendo ule ule, hadi alipopita kabisa mtaa huo. Alikwenda hadi alipofika mtaa wa mbele ambapo kulikuwa na uwanja wa michezo, hapo akaona magari kadhaa ya kifahari yakiwa yameegesha, bila kusita na yeye akaegesha gari lake na kutoka. Kwa hatua ndefu, imara na za haraka alitembea kuelekea alikoiacha ile nyumba.

Ilikuwa inagonga saa saba kasoro dakika kumi mchana wakati komandoo Twaha Mchoppa anawasili kwenye nyumba P-1 Butembo 309. Kati ya nyumba hii na nyumba ya jirani yake kulikuwa na uchochoro mdogo ambao ulifanya kijinjia ambacho mtu angeweza kutokea mtaa wa pili, ilionekana kuwa ni njia ambayo inatumika, hivyo alichukua kijinjia hicho. Wakati huo huo aliweza kusikia muungurumo wa radi na mawingu mazito yalionekana kujikusanya, hii ilimuambia kuwa muda mfupi ujao angetakiwa kuendelea na kazi yake kwenye mvua. Goma ni mji wa mvua nyingi, hilo analijua na akili yake ilishakubali hilo. Wakati akitembea kwa chati sana alikuwa akiziangalia kamera za CCTV jinsi zilivyokuwa zimekaa. Alikuwa amevaa magwanda ya kaki, halafu kwa juu alikuwa amevaa koti moja refu la kitambaa lililomfunika tokea juu hadi kwenye ugoko. Koti hili lilisaidia kuficha magwanda yake ambayo hata hivyo hayakuonesha yeye alikuwa wa upande upi, kilichosaidia tu ni kutoonekana kwa zana zake za kazi ambazo alikuwa amezipaki kwenye magwanda hayo. Japo koti lenyewe lilikuwa refu lakini vifungo vyake vilifunga hadi usawa wa mkanda wa kiuno, hivyo kuendelea chini lilikuwa likipepea tu kama mkia wa farasi. Alipofika sehemu ambayo mahesabu yake yalimuambia kuwa kamera ya upande huu na upande ule zisingempata aliruka kama nyani na kuparamia ukuta. Gloves ama kwa kiswahili tungesema mifuko ya mikono aliyokuwa amevaa ilimsaidia kuweza kunata vizuri kwenye ule ukuta mrefu aliokuwa ameupanda na kudumbukia kwa ndani ya ukuta, huku akiwa anacheza na kamera za CCTV alifanya miondoko yake kwa namna ambayo asingedakwa na kamera zile zilizokuwa zimefichwa vema. Kwa mtu wa kawaida asingeweza kujua kuwa kulikuwa na kamera za CCTV, zilikuwa zimewekwa kwa uficho kwenye dari la upande wa nje kuzunguka nyumba, zilionekana kama taa ndogo za mapambo zilizokuwa ndogo kama vifungo vya koti na zenye muonekano kama macho ya panzi.

Wakati anapiga hatua ya nne toka ukutani, aliangalia vema hatua zake, akarudisha hatua yake nyuma.
“Mafala sana hawa!” Mchoppa alitukana kwa kuwahusudu waliokuwa wameweka ulinzi kwenye nyumba hiyo. Bila shaka yeyote aliyekuwa ameweka ulinzi alishajua kuwa eneo hilo lisingekuwa chini ya CCTV kamera, hivyo kwa chini kwenye majani, majani yakawa yamekatwa kwa mtindo wa umbo la madini ya almasi, yaani ‘diamond style’, na macho pekuzi ya Mchoppa yakawa yameona pini moja iliyokuwa imejificha kwenye majani hayo yaliyokatwa vema. Ilikuwa pini ya kulipulia bomu, ina maana hatua ya tatu ingempeleka mtembeaji, ambaye angekuwa anakwepa CCTV kamera akanyage ile pini, ndio maana Mchoppa akarejesha mguu wake wakati anataka kumalizia hatua ya tatu.
Mchoppa akatabasamu, huku moyo wake unapiga kwa kasi.
Aliyeweka anajua hesabu, alishapima hatua ya tatu itakuwa hapa. Alishajua wapiganaji wengi ni warefu na hupenda kupiga hatua ndefu wanaponyata. Mchoppa aliwaza na kumsifia mtu aliyeweka ulinzi.
Unapokutana na fundi namna hii inatakiwa kufanya kinyume na matarajio. Mchoppa akajikumbusha. Hivyo akapiga nusu hatua, ikawa hatua yake ya tatu, halafu robo tatu hatua ikawa hatua yake ya nne. Alipoufikia ukuta akataka kusimama jirani na ukuta akasita, fanya kinyume na matarajio. Hivyo nusu hatua toka ukutani, akasimama pale pale. Akaangalia namna ambavyo anaweza kuingia ndani. Mara akaona kwa juu yake kulikuwa na dirisha. Dirisha la kioo. Kwa haraka akajua kuwa yeyote ambaye alikuwa amefanya ufundi wa kutega vitu eneo lile angekuwa ameona ule mwanya. Hivyo akafuta huo uwezekano. Kwa juu kabisa ya ukuta kulikuwa na ile sehemu ambayo wajenzi huweka kwa ajili ya kuingizia hewa, huwa ndogo kwa ukubwa wa msaafu mkubwa. Hapo akili yake ikaamua kufanya kitu ambacho alikuwa na hakika kuwa yeyote aliyeweka ulinzi asingefikiria. Aliingiza mkono kwenye moja ya mifuko ya gwanda lake, hapo akatoa kitu kama zile kamba maalum za kufanyia mazoezi ya kuruka. Alikielekeza kwenye dari la kwenye paa juu kabisa, akabonyeza kitufe fulani, kitu kama waya chenye kitu kama mshale kwa mbele kikafyatuka na kwenda juu na kujichomeka kwenye mbao ya darini kwa upande wa nje. Mchoppa akafanya kama anajivuta hivi ule waya ukaanza kumvutia juu. Hivyo akawa amekwea hadi juu kabisa. Alipofika kwenye ile sehemu ya kuingizia hewa ndani akapabomoa na kuondoa tofali moja zaidi, alikuwa na vifaa vya kutosha kufanya kazi hiyo bila kelele. Hapo akawa ametumbukia ndani. Alipoangalia kwenye dirisha alilosita kulitumia aliona waya maalum ukiwa umetandazwa kwenye lile dirisha ambao ulikwenda hadi kwenye bomu lililokuwa pembeni ya chumba kile.
“Damn it!” Alisema kwa kujigamba.
Hakukuwa na kitu kingine chochote chumbani mle. Alianza kuzungukia chumba kimoja baada ya kingine. Nyumba ilikuwa kubwa yenye vyumba vingi. Wakati akitembea kwenye kijinjia kimojawapo alisikia kama mashine ya faksi iko inafanya kazi, hapo alinyata kwenda kwenye hicho chumba. Aliweka kifaa chake maalum kwenye mlango halafu akasikiliza. Akajihakikishia kuwa hakukuwa na mtu, hivyo akafanya maarifa kuufungua mlango wa kile chumba ambao ulikuwa umefungwa. Baada ya dakika kadhaa alifanikiwa kuufungua mlango ule ambao kufungua kwake na kufunga kwake kulihitaji namba maalum.

Alipoingia tu ndani akakaribishwa na mashine iliyosema
“Welcome please, provide your passcode within two minutes” (Karibu, tafadhali unatakiwa kutoa nywila ndani ya dakika mbili).
Duuuh, hapo sasa!
Mchoppa akachachawa, akajua ilimaanisha nini kama angeshindwa kutoa nywila kama alivyotakiwa. Akili yake ikazunguka haraka haraka huku kijasho chembamba kikimtoka kwenye paji lake la uso. Hakutegemea angekutana na hali kama hii.
“Was**ge hawa!” Mchoppa alitukana kwa sauti ya kunong’ona. Dakika ya kwanza ikakatika. Wakati anafikiria cha kufanya mashine ikamkumbusha.
“You have only one minute to provide your passcode before it is too late!”(Una dakika moja tu imebaki ya kutoa Nywila kabla hujachelewa)
“Shiiit!” Mchoppa alisema sasa akiwa anahisi hewa inaanza kwisha kwenye kile chumba. Nguvu zikaanza kumwishia.

Mtunzi wa simulizi hii anapatikana kwa namba 0762204166

Kuendelea kusoma simulizi hii kuna njia mbili;
1. Unalipia sh5,000 kuja mpesa namba 0762204166. Utaelekezwa namna ya kuingia na kusoma yote.
2. Unanunua kitabu chake kwa sh10,000 toa kwa moja ya wauzaji wafuatao;

Kuletewa popote kwa gharama nafuu Dar es salaam- 0653254110
Dar - POSTA - ‭0755454152‬‬‬
Dar - KARIAKOO- ‭0653254110‬
Dar-Kinondoni - Biafra - ‭065 542 8085‬‬
Dar - U B U N G O - ‭067 868 3278‬‬
Arusha -‭ 0757690302‬ au ‭0656744390‬‬‬
Mwanza City Mall - 0744657361
Mwanza - ‭ ‭0715057315‬ au 0754057315‬‬
Moshi - ‭ ‭0754963999 au 0654241700‬‬
Kilindi- 0713731821
Kasamwa - ‭068 810 2030‬‬
Dodoma -‭ 0715368220‬‬
Kibondo - 0655555750
Mpwapwa - 0715368220
Mbeya - 0754091481
Babati ‭0787513647‬
Maswa - 0766048469
Kasulu- ‬ 0655555750
Bukoba- ‭ 0675 309 841‬
Namanga- 0757690302
Handeni- 0713731821
Zanzibar - 0652084191
Lindi - 0716725662
Kemondo- 0675 309 841
Kigamboni - 0755454152
Tukuyu- 0753914696
Bariadi- 0766048469
Bunda - 0759142940
Sengerema - ‭068 810 2030‬‬
Ifakara - 0621075891
Mtwara - 0712962005
Muleba- 0675 309 841
Karatu- 0787513647
Zanzibar - 0713251717
Bihalamulo- ‭068 810 2030‬
Chunya- ‬ 0753914696
Mutukula - 0675 309 841
Arusha -‭ 0757690302‬‬
Sumbawanga- 0764123845‬
Moshi - ‭ ‭0754963999 au 0654241700‬‬
Morogoro -‭ ‭ ‭0621075891‬‬‬
Longido - 0757690302
Kahama - ‭0753 574 124‬‬
Chato - ‭068 810 2030‬‬
KIGOMA - 0655555750
Geita - ‭ ‭068 810 2030‬‬
Mbozi - ‬ 0753914696
Rudewa- 0753705024‬
Songea - 0762353918
Tabora - 0765052507
Mpanda - 0764123845‬
Kilombero - 0621075891
Karatu - 0757690302
Dodoma -‭ 0715368220‬‬
Ushirombo - ‭0753 574 124‬‬
Musoma - 0759142940
Katoro - ‭068 810 2030‬‬
Morogoro -‭ ‭0621075891‬‬‬
Songwe - 0753914696
Iringa -‭ 0753705024‬‬
Tunduma - ‭0764123845‬‬
Kondoa - 0715368220
Ngara - 0655555750
Kagera - ‭0758274733‬‬
Mvomero - 06210758914
Kakora - ‭068 810 2030‬‬
Tanga - ‭0713731821‬‬
Tarime - ‭0759142940‬
Bahi- ‬ 0715368220
Bukombe - ‭068 810 2030‬‬
Shinyanga - ‭0766048469‬‬
Lushoto - 0713731821
Singida - ‭0764 393 260.‬

M P I G I E MUUZAJI AKUELEKEZE ANAPOUZIA
Ukiuliza sehemu halafu ukaambiwa vimekwisha tafadhali nitaarifu kwa namba 0762204166 ili nifanye utaratibu wa kutuma vingine.

Kama havijafika wilaya yako basi angalia eneo la jirani vilipofika halafu wasiliana na muuzaji ili akutumie kwa basi.


Ili uweze kuendelea kusoma Tuma Tsh. 5000 kwenda namba +255 762 204 166 ili uweze kusoma kitabu SAA 72


RIWAYA ZA KUSISIMUA NA MAFUNZO

PATAPOTEA
PATAPOTEA
PATAPOTEA

Patapotea © Japhet Nyang’oro Sudi, 2019 ISBN 978-9987-794-08-9 1 Taarifa ziliponifikia kwanza nilizipuuzia. Niliendelea na shughuli zangu kwani niliziona kuw

MDHAMINI
MDHAMINI
MDHAMINI

SURA YA KWANZA Alikohoa tena na tena, kihohozi cha taabu, huku uso wake ukionyesha alikuwa akipata maumivu makali. Alijitahidi kuyadhibiti makohozi yake kwa kufunika kinywa c

OPERESHENI PANAMA
OPERESHENI PANAMA
OPERESHENI PANAMA

Operesheni Panama Ilikuwa siku ya 18 ya mwezi Machi mwaka 2003 katika jiji la Dar es Salaam, Tanzania, wakati taarifa ilipomfikia. Kilipomfikia, kilikuwa kama tone la maji

PATASHIKA
PATASHIKA
PATASHIKA

KITABU: PATASHIKA 1 Usiku wa Kizaizai ALISHTUKA toka usingizini. Akajituliza pale kitandani kwa sekunde kadhaa, masikio yake yaliweza kusikia moyo wake

SAA 72
SAA 72
SAA 72

S A A 7 2 Februari 25, 2003 Bogoro – Buni, DRC Msichana wa miaka 15 hivi, akiwa na majeraha mazito mwilini alizidi kujilazimisha kupiga hatua kwenye mtaa ul